Mwenyekiti wa kikosi cha Arsenal Tanzania Said Tully mwenye miani yeye amejigamba kwa kuanika majina ya wachezaji wa Arsenal kuwa ni Majuto Omari, Idd Janguo, Okwi, Mussa Mgosi na Heavy D pia kutakua na nafasi za kina dada kw timu hiyo.
Aidha hadi sasa tayari ratiba ya mechi hiyo iko tayari ambapo timu za kundi A ni Real Madrid, Manchester United, Chelsea na Liverpool . Wakati timu za kundi B ni Milan , Inter Milan , Barcelona na Arsenal. Duda alisema mechi hizo ambazo zitachezwa nusu uwanja na kwa muda wa dakika 20 huku timu itakayoibuka na ushindi watapata zawadi ya sh. Mil.1 na wapili watapata sh. 500,000. Aidha Mratibu huyo aliwataja baadhi ya viongozi wa timu hizo kuwa ni majina kuwa ni Clifford Ndimbo Mwenyekiti wa Chelsea Tanzania, Frank Christopher Mwenyekiti Manchester United. Wengine ni Said Tully Mwenyekiti wa Arsenal Tanzania , Wilfres Kidau Inter Millan, , Rashed Nurden Katibu Msaidizi Liverpool na Adam Gwao Mwenyekiti Liverpool. Mashabiki wa timu zote ambao watavaa jezi wataingia Leaders bila kiingilio ila kwa wale ambao hawatakuwa na jezi watalazimika kulipa kiingilio cha sh.3000 mlangoni. Tamasha hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Serengeti (SBL). Kama ilivyo kawaida katika mpira kutoleana tambao ambapo Ndimbo aliwatishia nyao wenzake kwa kutaja wachezaji wake wawili ‘Professional’ kuwa ni Kalli Ongala na Ivan Knezevic.
0 Comments