Je, unamjua Amanda Annan? Amanda ni British Super Model na katika ulimwengu wa ulimbwende anajulikana kama ‘Rebel Niece’, kwa sababu yeye Amanda (Kofi Atta Annan (baba mdogo wa Amanda) ni Mwanadiplomasia toka Ghana ambaye ni mtu wa 7 kushika wadhifa wa cheo cha Secretary-General wa United Nations kuanzia 1 January 1997 hadi 31 December 2006.) amezaliwa kwenye familia ya wasomi, wanasiasa na Wanadiplomasia, lakini alipotimiza umri mdogo wa miaka 17 akajikita kwenye fani ya uanamitindo, uigizaji na ulimbwende tofauti na matarajio ya wazee wake.
Amanda aliliona jarida la Shear Magazine akiwa matembezini nchini Marekani kwa rafiki yake ambaye in dada yetu wa Kibongo aitwaye Pendo Nyonyi anayeishi katika Jiji la Los Angeles.
Agent/manager wake akapenda wazo la Amanda kutupatia nasi historia yake kwa ufupi na kuwapa moyo kina dada wa Kibongo mbinu za kujikita katika ulimbwende na kutokukata tamaa katika kufanya kile kitu ambacho moyo unapenda, na pia anaeleza kwa kina kuwa mafanikio hayaji bila kujituma, uvumilivu na ujuzi pia.
Pata nakala yako ya Toleo jipya la Kumi maana liko mitaani sasa uweze kusoma story ya kusisimua ya Amanda, kazi zake alizofanya za kuisaidia jamii ya wanawake Afrika, siri zake za urembo, utunzaji wa mwili, ngozi na nywele. Pia ndani ya toleo hili, utapata kujua historia fupi ya 'Legend' Issa Michuzi katika page maalum ya brothers, mahojiano na Ankal Michuzi amewapa wasomaji historia yake ambayo watu wengi hawaijui na yeye binafsi hajazitoa katika blog yake. Nunua nakala yako sasa kwa TSh.5,000 tu!
0 Comments