Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mikoa na Tawala Shirika la Nyumba nchini (NHC), Raymond Mdolwa akisimamia zoezi la kuwatoa wapangaji ambao ni wadaiwa sugu, hapa ilikuwa ni leo asubuhi maeneo ya Posta Jijini Dar es Salaam. Huu ni mpangi mkakati wa NHC kuwatoa wapangaji ambao wamekuwa wagumu kulipa kodi ya pango.Zoezi hilo lilianzia Mtaa wa Zanaki na Libya kwa kampuni ya Tom’s Ltd majira ya saa nne asubuhi na kufuatiwa na kampuni ya JV Enterprises iliyopo Mtaa wa Makunganya. Akizungumza na waandishi wa habari wakati zoezi likiendelea,Mndolwa alisema zoezi hilo limekuja baada ya siku zilizotolewa kumalizika na wahusika kutshindwa kutoa taarifa zozote huku akisisitiza zoezi hilo limepangwa kufanyika kwa wapangaji wa NHC nchini kote huku wakiwa wanaanza katika majengo ya biashara.Hizi ni baadhi za samani zilizotolewa nje ya moja ya ofisi ambayo ilipanga katika jengo la NHC. Wafanyakazi na wananchi wakiwa nje ya jengo ambalo wametolewa wapangaji wadaiwa sugu.
NFRA SONGEA YANUNUA TANI ZAIDI YA 72,000 ZA MAHINDI MKOANI RUVUMA
-
Na Mwandishi Wetu,Ruvuma
WAKALA wa Taifa wa hifadhi ya chakula(NFRA)Kanda ya Songea mkoani
Ruvuma,imenunua tani zaidi ya 72,000 za mahindi kutoka kwa ...
4 hours ago
0 Comments