Pichani kutoka shoto ni Hamisi Kayumbu Amigolas, Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka Luiza Mbutu na aliyepakatwa ni Khadija Kimobitel baada ya kutangazwa kurudi Twanga.
***************************************************
Aliyekuwa Kiongozi wa bendi ya Extra Bongo Aambayo Mkurugenzi wake ni Ally Choki Khadija Mnoga ‘Kimobitel’ amerudisha mabegi yake katika bendi ya The African Stars Twanga International ‘Twanga Pepeta’ na kutangazwa kujiunga na bendi hiyo leo asubuhi.
Kimobitel ambaye amekiri kwa ndimi yake mbele ya wanahabari katika mkutano uliofanyika jana kuwa ameamua kubwaga manyanga kutokana na kutothaminiwa na kutolipwa mshahara na marupurupu.
Alisema mimi binafsi nimeguswa na kitendo cha Choki kuchukua wanamuziki nane kutoka Twanga na kuwalipa vizuri fedha nyingi wageni na kututosa sisi wakongwe ambao tumesota na bendi hii bila kulipwa mishahara.
Kimobitel ambalo ni jina lake la umaarufu aliendelea kwa kusema kuwa , alisikitishwa zaidi hasa pale alipoambiwa yeye kama Kiongozi wa bendi awafukuze kazi wanamuziki saba wa Extra Bongo ili wawapishe wengine wapya ambao ndiyo hao nane waliotoka Twanga.
Alisema aliumia sana alipopewa rungu la kuwafukuza kazi wasanii hao huku akimtaja Greyson Semsekwa , Dasu ,Idd, Mfaume, Pink na wengine wawili ambao walikuwa wapya katika bendi.
“Chochote kinachotokea ASET kiwe kizuri au kibaya kuwa napenda kukifuatilia kwa sababu huku ndiko nililotokea mimi ambapo nilianzia katika bendi ya Chumvichumvi hivyo hapa ni nyumbani nimeamua kurudi nyumbani”alisema.
Aidha amesema hivi sasa katika bendi ya Extra Bongo wasanii wengawanyika kutokana na roho kuwauma kwa kuona wenzao wamechukuliwa na kulipwa fedha huku walioifikisha bendi hiyo hapo ilipo wakiachwa bila kuthaminiwa.
Akithibitisha hayo Asha Baraka alisema kwamba kuna kundi la wanamuziki kutoka Extra Bongo akiwemo Semsekwa walifika katika Ofisi za ASET kuomba kazi huku yeye akiamua kumchua Kimobitel peke yake.
Khadija akieleza mambo mbalimbali kuhusu Extra Bongo mbele ya wanahabari kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari hawapo pichani leo asubuhi.

0 Comments