ASHA BARAKA AMJIBU CHOKI, ASEMA TWANGA SIYO BENDI YA MSIMU

Kutoka kushoto ni God Kanuti, Kiongozi wa bendi Luiza Mbutu,Venance na Khadija Kimobitel.
Asha akimtambulisha God Kanuti kwa wanahabari ambaye wazazi wake wamemzuia asiende kujiunga na Extra Bongo na kurudisha fedha alizopewa. Asha Baraka akifafanua jambo kulia kwake ni Luiza.

Ikiwa ni siku tano tu tangu bendi ya Extra Bongo wanyakue wanamuziki wananne wa bendi ya Twanga Internationa Mkurugenzi wa Kampuni ya The African Stars Entertainmnent (ASET),Asha Baraka ameibuka na kusema kuwa hawatetereki na watabaki kileleni.
Asha ambaye pia ni mmoja kati ya wamiliki wa bendi ya Twanga International ‘Twanga Pepeta’, ameyasema hayo leo asibuhi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi za ASET Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
“Twanga ni mwenye wenye maembe matamu hivyo kwa kitendo cha Ally Choki kuchukua wasanii wa bendi hii sishangai kwani alianza chochoko hizo muda mrefu na wapo baadhi ya wasanii waliolipwa fedha muda mrefu hivyo tulijua kuwa wataondoka”.
Asha anaendelea kwa kusema kuwa hana kinyongo na wasanii walioondoka bali anawaombea dua njema na kutaka watumie vyema fedha walizopewa kwa sababu ni za msimu siyo endelevu.
Twanga hatutaki malumbano sanaa ni vipaji hivyo hapa ASET wapo wasanii wengi ambao ni wasomi lakini wameamua kubobea katika sanaa na ukikata mti unapanda mti wale wameondoka wengine wanaendeleza gurudumu.Wakati huohuo amesema kwamba bendi hiyo haiendeshwi kwa majina au kwa jina la msanii fulani kwa sababu wasanii wake wote ni nyota na wana uwezo sawa hakuna makundi kama wengi wanavyoweka matabaka kwa wasanii.
“Hapa Twanga kila mtu analipwa mshahara hakopwi mtu au kumshusha huyu ukampandisha msanii mwingine” anasema.
Akizungumzia kuhusu bendi ya Extra Bongo kuchukua wasanii wake alisema kuwa anahakika anachokisema kuwa hiyo ni bendi ya msimu kwani anajua kwamba ipo siku itavunjika kama ilivyovunjika ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza.
“Nasema hivi Choki hatonikomesha mimi , mimi ni mwanasiasa, mfanyabiashara ninafedha kumshinda yeye na hata huyo mama ambaye analetafujo hivi sasa katika biashara ya muziki muziki siyo chuki kama wanavyofanya wao labda waje wanichome kisu hapo kweli lakini vinginevyo hawaniwezi” alisema Asha Baraka.
“Wanahabari hebu angalieni historia za bendi zoote hapa nchini Twanga haijawahi kufa lakini Extra Bongo iliwahi kufa na sasa wameibuka huku wakitegemea kunyakua wasanii wa Twanga ili walikamate soko,jambo lisilowezekana Twanga inahistoria yake” alisema Asha.
Wakati huohuo alimpongeza Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (THT),Ruge Mutahaba kutokana na jinsi alivyoweza kuwaibua wasanii na kulikamata soko, pia amempongeza na Mkurugenzi wa Benchmark Productions Rita Poulsen kutokana shindano lake la Bongo Star Seach (BSS), wenye vipaji wapo kwa nini watu hawataki kuwavumbua walikotoka na kuchukua wasanii wa wenzao?
Aidha amemsifu msanii mdogo kuliko wote katika bendi hiyo Martin Kibosho kutokana na uamuzi wake wa kutoihama bendi hiyo aliseme, namsifu Kibosho kwani mara alipoitwa na kupewa fedha kiasi cha sh. mil 6 alizigawa katika bahasha na kulinganisha patp lake la mwaka na kugundua kwamba hazitaweza kukidhi matakwa yake ya kila siku licha ya kwamba amekuwa akipokea vitisho kila kukicha jambo lililopelekea kuzima simu yake ya kiganjani.
Mwisho Asha amemtangaza Kassim Mohammed (Super K) , kuwa kiongozi wa wanenguaji wa kiume ambapo ameri8thi mikoba ya Nyamwela na Lilian Tungaraza ‘Internet’ kuwa kiongozi wa wanenguaji wa kike.
Hamis Kayumbu ‘Amigolas’ ambaye Meneja Matukio na Uhusiano, Kiongozi wa bendi ni Luiza Mbutu akisaidiwa na Saleh Kupaza ambaye pia ni Mhakiki wa tungo za nyimbo.

Post a Comment

0 Comments