WATANZANIA WAMWIBIA MMAREKANI

Leo asubuhi wakati nikielekea ofisini katika round about ya Azam iliyopo katika Mtaa wa Mkwepu Jijini Dar es Salaam nilisikia nikisalimiwa na dada huyu wa kizungu nami nikamjibu na nilipomtupia jicho nikamwona ni mtu anayehitaji msaada nikasimama na kumsikiliza.Hivyo moja kwa moja akaniuliza wapi kilipo kituo cha Polisi Kati yaani Central Police , nikamwambia huku unakoelekea siko twende nikipeleke.Basi safari ikaanza na wakati tukiwa njiani nikamwuliza tatizo linalompeleka Polisi akasema kaibiwa kila kitu Mkoani Songea alipokuwa safarini kwenda Malawi Looh yaani ma'bro wa Bombi Nyumbi ndo wamekuwa wakora noma. Kusema kweli nilijisikia vibaya ghafla na kuona aibu kwani doa kwa nchi tayari.Wakati safari ikiendelea nikajitambulisha majina yangu yote na kumwambia kazi yangu wakati huo tulikuwa nje ya jengo la ofisi yetu Club Bilicanas akasema anaomba kopi ya gazeti hivyo nikampandisha ghorogani tukaenda kuchukua kopi ya gazeti na kumpatia alifurahi saana mimi nikawa nainjoi tu kuona mtu anafurahia na kuthamini kazi za watu wengine hiyo ni roho nmzuri na watu wachache wako hivyo jamani uwongo uwongo KWELIII.
Anaitwa Jill Dryden ametoka Texas Marekani, kaibiwa Passport yake,Camera, na fedha hivi sasa anaishi kwa jamaa / marafiki zake Masaki Jijini Dar es Salaam.Nilimwuliza kama aliwahi kuja Afrika , akajibu hii ni mara yake ya pili mara ya kwanza alikwenda nchini Ghana miaka miwili iliyopita na safari hii ndiyo akaamua kuja Tanzania ambako ni mwendelezo wa safari zake za kitalii barani Afrika.Akikamilisha mambo yake atakwenda Malawi, Afrika Kusini na baada ya hapo atarudi kwao Marekani. Niliguswa na kadhia aliyoipata shoti huyu ambapo nilijitolea kutembea naye kwa miguu kutoka mkwepu hadi Central Police ambapo alikwenda kuandikisha maelezo yake.Safari njema Jill na mungu atakusaidia utainjoi lakini hii ndiyo Afrika bana watalii kuweni makini kwani wapo watu wameumbwa kuishi kwa kupora vitu vya watu.

Post a Comment

1 Comments

jilledaway said…
Hi Khadija! I just want to tell you that I am back home in America. Thank you for all your help!

Jill