CCM WASUSA MAZISHI YA MUASISI WA TANU ALIKUWA MSANII MAARUFU TABORA

Na Mwandishi Wetu Tabora
Muasisi wa kundi la Muinamila lilokuwa likipiga ngoma zake katika mtindo wa Hiari ya Moyo inayochezwa na Kabila la Wanyamwezi ambao ni wenyeji wa Mkoa wa Tabora Kabhunga Kakwesella Kadatta amefariki dunia.
Licha ya kuwa muasisi wa kundi hilo pia marehemu Kabhunga ambaye alikuwa Mkuu wa ngoma za jadi ya Waswezi Mkoani Tabora (Mashujaa wa Nyanyembe) ambaye ndiye alikuwa akiliandaa kundi la Waswezi kuja Jijini Dar es Salaam katika tamasha la sikukuu ya kuenzi utamaduni wa Wanyamwezi na Wasukuma iliyopangwa kufanyika Aprili mosi mwaka huu katika Viwanja vya Karimjee.
Kaka wa marehemu Kadatta Kakwesella alisema kuwa kifo hicho kimeacha pengo kubwa siyo tu katika familia bali kwa Waswezi pamoja na Wanyamwezi wote kwa ujumla.
Aidha marehemu alikuwa miongoni mwa waliokuwa wasisi wa Chama Cha TANU Mkoani Tabora.
Kadatta amesema amesikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Tabora pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutohudhuria wala kutuma mwakilishi katika msiba huo na kutotoa salamu za rambirambi ikiwa ni pamoja na kutotambua mchango wa marehemu katika chama hicho.
“Msiba huu ulikuwa ni wa mtu muhimu na maarufu katika Chama hapa Mkoani Tabora, alifariki ghafla baada ya kuanguka chooni Desemba 24 na kuzikwa Desemba 26 katika makaburi ya Mwinyi Tabora”.
Marehemu alizaliwa 1936 katika kijiji cha Kapalamansa Wilayani Urambo mkoani Tabora.
BLOG HII INATOA POLE KWA WAFIWA WOTE NA WANYANYEMBE WOTE.INNALILA H WAINAILAIH RAJIUN.

Post a Comment

0 Comments