WANYAMWEZI,WASUKUMA KUFANYA TAMASHA NA KONGAMANO LAO

*********************
Kamati ya maandalizi ya kongamano na tamasha la makabila makuu ya Wanyamwezi na Wasukuma (UWAWATA) wametangaza majina ya wanakamati wake imefahamika.
Akizungumza jana na Mratibu wa kongamano na tamasha hilo Kadatta Kakwesella Kasula Kalele Kidula, Anamtaja Mwenyekiti wa Kamati ni Jaji Mark Bomani huku Makamu wake akiwa Mbunge wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora Rostam Aziz.
Mlezi Jamii Waziri wa Ushirikiano Afrika Mashariki pia Mbunge wa Jimbo la Urambo Mkoani Tabora.
Huku Balozi S.P Mayunga na Wallace Mayunga wote wameteuliwa kuwa washauri wa kamati hiyo.
Aidha Mkurugenzi wa Habari na Ushirikiano katika Kampuni ya Serengeti Teddy Hollo Mapunda, Shy Rose Bhanji na David Kizito wote ni Washauri na wadhamini katika tamasha hilo.
Nafasi ya Ushauri na Utamaduni imekwenda kwa Shadrack Kavalambi huku Kansolele akitajwa kuwa Mshauri na Uhusiano.
Wajumbe katika kamati hiyo ni Dotto Masudi, Khadija Kalili Kanyanyila licha ya kuwa mjumbe pia atasimamia suala zima la Habari ,Agather Mzukira, Johari Masengense, wengine walitajwa kwa jina moja ni Richard, F.Gembe na Buhini.
Kadatta alisema majina haya yalipendekezwa na kuteuliwa na waasisi wa UWAWATA ikiwa ni katika kufanikisha tamasha hilo linalotarajiwa kuwa la kihistoria hapa nchini kabla na baada ya kupata uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.

Post a Comment

0 Comments