Akizungumza jana na waandishi wa habari Mwenyekiti wa UWF ,Mwate Nnauye Madinda alisema thamani ya hundi zote zilizotolewa jana ni shilingi milioni 10.
Alisema tangu waanzishe umoja huo nuaka nitano iliyopita wameweza kutoa msaada kwa wanafunzi 40 huku lengo lao likiwa ni kusomesha watoto 50.
“Tunatoa fedha zetu binafsi mifukoni na lengo kubwa ni kutoa elimu kwa mtoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao,watoto wa kike ambao wengi ni yatima na wenye wazazi wasiokuwa na uwezo” alisema Madinda.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kituo Cha Utamaduni Cha Urusi Jijini Dar es Salaam, Maryan Ajmy
Aliongeza kwa kusema kuwa katika kujiridhisha kweli wazazi hawana uwezo huwa wanazitembelea familia za watoto na kuona hali halisi ili msaada uweze kuwafikia walengwa na siyo vinginevyo.
"Watoto wengi wa kike wanatamani kufikia malengo waliojiwekea maishani pia wanauwezo mkubwa darasani lakini kutokana na ukosefu wa fedha unaozikumba familia zao wanashindwa kuendelea hivyo tunajitahidi kutimiza ndoto zao kwa kuwapa elimu kwa kuwachangia ada " alisema Bi. Madinda.
Alisema, ada hizo wanazolipa ni kulingana na ada ya shule wanaposoma watoto hao ambapo baadhi yao wanasoma shule za watu binafsi na wengine wanasoma katika shule za serikali ambapo na mwanafunzi mmoja anasoma chuo.
Bi. Madinda alisema wanawasomesha wanafunzi hao hadi mwisho wa masomo yao ambapo amesifia uwezo wawanafunzi hao wanaouonyesha katika matokeo yao ya darasani.
Mwate Madinda Kushoto akikabidhi hundi kwa mwanafunzi huku akishuhudiwa na mwanachama wa UWF Maryam Shamo.
0 Comments