Social Icons

Wednesday, January 5, 2011

MIAKA MITANO YA THT KUFANYIKA MLIMANI CITY JANUARY 11 TIKETI NI KWA WATU 400 TU

Mwasiti ataonyesha Swagga zake siku hiyo.
Mataluma licha ya kuwa na ngona nyiki kali pia takuonyesha jinsi anavyomudu kusakata kiduku siku hiyo Lina msanii wa kike ambaye ni moto wa kuotea mbali atakamua siku hiyo.
Ditto ataachia ngoma yake ya Wapo na nyinginezo katika albamu yake siku ya uzinduzi.
Barnaba anakuja na albamu aliyoipa jina la Kichwa Changu Usipime.

Naye Kijana Amini tamwaga masongi yake yaliyomo katika mkebe wake alioupa jina la Yameteka Dunia.

*******************

Maandalizi ya kusherehekea miaka mitano ya Nyumba ya Kuvumbua vipaji nchini Tanzania House Of Talent (THT), imekamilika hivyo wadau wametakiwa kukaa mkao wa kupata raha ya kufungua mwaka katika onyesho la aina yake ifikapo Januari 11 mwaka huu.Itakuwa Jumanne Ijayo yaani siku ya mkesha wa sikukuu ya Mapinduzi Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Msemaji wa THT Kemmy Mutahaba ilisema.

Kiingilio kitakuwa sh. 30,000 huku uongozi wa THT umepanga onyesho hilo kuwa na watu 400 tu katika ukumbi hivyo mashabiki wametakiwa kuchangamkia katika kununua tiketi ili waweze kupata fursa ya kushuhudia tamasha hilo.
Mutahaba alisema mbali na maadhimisho ya miaka mitano pia watazindua albamu sita kwa mpigo za wasanii wanaotamba hivi sasa ambao ni zao la THT ambao ni Mwasiti, Amini, Dito, Barnaba, Lina na Mataluma. Yaani nikana jinsi makasha yanavyoonekana hapo juu.

Licha ya kuzindua albamu zao wasanii hao wataudhihirishia umma utakaofika ukumbini hapo kwamba wao ni wakali kwa kuonyesha shoo ya aina yake usiku wa siku hiyo.
Aliongeza kwa kusema kuwa mambo mengi mapya kuhusu THT yataanikwa siku hiyo.
Bendi ya Odama itatumbuiza.

Wadau tutawatangazie sehemu ambazo tiketi za onyesho hilo zitakapouzwa.

No comments:

 
 
Blogger Templates