Social Icons

Thursday, January 6, 2011

FM ACADEMIA KUVAMIA UK BONGO KESHO

Bendi ya muziki ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ Ijumaa Januari 7 wanatarajiwa kufanya onyesho la aina yake kwa wakazi wa Ukonga na viunga vyake.

Akizungumza na Tanzania Daima jana Meneja wa bendi hiyo Kelvin Mkinga alisema watapiga shoo ya aina yake katika ukumbi wa Wenge uliopo , Mombasa Ukonga.

Mkinga alisema onyesho hilo ni maalum kwa kutoa salamu za mwaka mpya kwa mashabiki wake na wakazi wa eneo hilo.

Alitaja kiingilio kitakuwa sh. 5,000 tu.
Katika onyesho hilo FM Academia watamtambulisha muimbaji wake wa kutumainiwa Mule Mule FBI ambaye amerudi tena kundini baada ya kuwa pembeni ya bendi hiyo kwa muda.

Aidha wakazi wa Ukonga watapata futsa ya kusikilishwa na kuchezewa nyimbo zinazotamba hivi sasa za ‘Jasmin’, ‘Mwili Wangu’, ‘Mgeni’ na ‘Sikutegemea’

Kadhalika watatambulisha wimbo wao wa mpya unaokwenda kwa jina la ‘Chuki ya Nini’. Baada ya Onyesho hilo Jumamosi watakuwa katika Kijiji Cha Makumbusho Dar es Salaam.

No comments:

 
 
Blogger Templates