KILIMANJARO STARS YAZINDUKA SASA KUIONA ROBO FAINALI YA TUSKER CHALLENGE CUP 2010





Uzalendo wa Watanzania katika soka kumbe kikwazo kilikuwa ni kiingilio (Picha kwa kisani ya http://www.jiachie.blogspot.com/) .
Mshambuliaji watimu ya Kilimanjaro Stars, Thomas Ulimwengu (kulia), akimkabili Anwar Ibrahim wa Somalia, timu hizo zilipomenyana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika michuano ya Tusker Challenge 2010.(Picha Zote nawww. Chachandu Daily.blogspot.com).




Mshambuliani wa timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars,Nurdin Bakari akipachika bao la tatu dhidi ya Somalia mara baada ya kupata krosi maridadi kabisa kutoka kwa Mrisho Ngasaa.hadi mwisho wa mchezo Kilimanjaro stars 3-0 dhidi ya Somalia.

Kiungo wa kati wa Kilimanjaro Stars,Henry Joseph akipena misuli na mchezaji wa timu ya Somalia katika mechi ya mashindano ya Tusker Challenge Cup 2010 yanayoendelea kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa pembeni wa timu ya taifa ya Kilimanjaro stars,Mrisho Ngassa akionyesha umahiri wake mbele ya beki wa timu ya taifa ya Somalia katika mchezo uliopigwa leo ndani ya uwanja wa Taifa jijini.Kilimanjaro stars iliweza kuibuka kidedea kwa kuichapa timu ya Somalia mabao 3-0. Leo uwanja umejaa kwani kulikuwa hakuna kiingilio jabo lililoleta hamasa uwanja ukajaa hakukuwa na mapengo kama ilivyokuwa hapo awali.

Kocha wa timu ya Kilimanjaro stars,Jan Paulsen akifatilia kwa makini mchezo huo.

Post a Comment

0 Comments