Mwanamuziki nyota wa barani Afrika, Bozi Boziana anatarajiwa kuwasili nchini Novemba 25 kufanya maonyesho mawili akiwa na bendi ya African Stars maarufu, Twanga Pepeta.Maonyesho hayo yamepangwa kufanyika Novemba 27 kwenye ukumbi wa Mango Garden na siku inayofuata kwenye viwanja vya Leaders Club katika bonanza la kila siku ya Jumapili maarufu kwa jina la SSB.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET), Asha Baraka amesema leo kuwa hatua ya kufanya onyesho na mwanamuziki huyo mkongwe inatokana na mpango wao wa kujitangaza katika soko la kimataifa.Baraka alisema kuwa mara baada ya maonyesho hayo, wanamuziki wengine wa Bozi Boziana wataondoka nchini na mkongwe huyo kubakia hapa nchini akiandaa albamu mpya ambayo atairekodi akiwa na wanamuziki wa bendi yake.Alisema kuwa albamu hiyo itakuwa na lugha mchanganyiko ya Kilingala na Kiswahili na baada ya kukamilika utunzi wake, itakwenda kufanyiwa ‘mixing’ nchini Ufaransa.“Bozi Boziana ataimba Kilingala na baadhi ya maneno kuimba Kiswahili, wanamuziki wetu watimba Kiswahili na Boziana kuimba ubeti huo huo Kilingala, lengo hapa ni kupromoti lugha yetu kwani naamini albamu hii itauza DR- Congo na nchi nyinginezo,” alisema Baraka.Asha ambaye anajulikana kama mwanamke wa chuma “Iron Lady” amewaomba wadhamini mbali mbali kujitokeza kusaidia kufanikisha kwa maonyesho hayo mawili na maandalizi ya albamu hiyo.Alifafanua kuwa bendi yae pia itaendelea na maandalizi ya maandalizi ya albamu mpya ambapo mpaka sasa wamekwisha kamilika jumla ya nyimbo nne.
DKT. NCHEMBA AMUAGA BALOZI WA MAREKANI NCHINI
-
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa
Tanzania ina thamini mchango mkubwa wa Taifa la Marekani ka...
9 hours ago
0 Comments