MAONYESHO YA WIKI YA VISIWA VYA SHELISHELI KUFANYIKA TANZANIA


Kutoka kushoto Mratibu Sauda Simba Kilumanga katikati ni Balozi wa Heshima wa Visiwa vya Shelisheli Maryvonne Pool na anyefuata ni Mama Hellen Sweya.Wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya maadhimisho ya visiwa vya SheliSheli itakayo fanyika kati ya Novemba 15-20.
Visiwa vya Shelisheli kushirikiana na Tanzania katika kukuza Uchumi wa Utalii wa ndani na nje kwenye wiki ya maonyesho itakayofanyika kuanzia Novemba 15 hadi 20.

Akiongea na waandishi wa habari jana Maelezo jijini Dar es Salaam, Balozi wa Heshima wa visiwa hivyo nchini Maryvonne Pool alisema kuwa lengo maonyesho hayo yatasaidia kukuza mahusiano ya karibu baina ya Tanzania na Shelisheli ambayo uchumi wake umekuwa kwa kiwango kikubwa kupitia nyanja za Utalii wa ndani na nje.

“Lengo ni kukuza uchumi ususani nyanja ya Utalii baina ya nchi hizi mbili Tanzania na Shelisheli, hivyo wadau mbalimbali watajumuika pamoja na kushuhudia vitu mbalimbali vya Shelisheli vitakavyokuwa vikionyeshwa na kupata kujifunza pamoja na kupatiwa ujuzi wa jinsi visiwa hivyo vilivyofanikiwa kiuchumi kupitia utalii” alisema Maryvonne.

Katika wiki hiyo itakayoanza kuanzia Novemba 15 hadi 20 itakuwa na maonyesho mbalimbali ikiwemo vyakula vya watu wa visiwa vya Shelisheli pamoja kuburudani mbalimbali sambamba na meli maalum ya visiwa hivyo itakayokuja nchini na watu mbalimbali watapata kutembelea visiwani humo.

Post a Comment

0 Comments