LICHA YA MVUA KUBWA KUNYESHA JANA DAR ES SALAAM BONANZA LA LEADERS CLUB LILIENDELEA KAMA KAWAIDA

Mwali Ibrahim kushoto na mimi tukiwa katika bonanza hilo.
Wacheza Shoo wa bendi ya Twanga wakiwa wamepozi kwa picha mara baada ya kuachia nyonga.

Kutoka kushoto Mwali Ibrahim,Kiongozi wa bendi ya Twanga Luiza Mbutu,Mama Lifatash na Angel Bushoke .

Victot Mkambi bila huyu utamu hauwezi kukolea au siyo mwache apapase banaa.

Pambo jipya la jukwaa katika bendi hiyo akiwa ametokea umangani makamuzi yake siyo ya kitoto.


Mwalimu wa timu ya TASWA FC Ibrahim Massoud 'Maestro' mwenye kofia na anayejipendelea ni Moland.
Mimi na Mwenyekiti wa timu ya TASWA FC Majuto Omary hapa tulikifuatilia 'Sugua Kisigino' .


Wasdau mnamkumbuka Adolph Mbinga?Mwenye kofia huyo ni miongoni mwa waasisi wa bendi hiyo.
Tamu ya mdundo ni kuudemkia kama tunavyomwona mpiga ngoma huyu mdomo upande mambo ya mzuka.

Rapa na muimbaji wa bendi ya Twanga Saulo Fagurson akiwa na Luiza hapa wakipata mapumziko mafupi.


Roggert Hegga 'Caterpiler' ambaye ni muimbaji wa bendi ya muziki wa dansi ya The African Stars almaarufu kama Twanga Pepeta leo usiku watatoa burudani katika mkesha wa sikukuu ya Eid El Hajjj itakayoadhimishwa duniani koteJumatano.

Akizungumza na Tanzania Daima jana Meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter alisema kuwa bendi hiyo itatumbuiza katika Klabu ya Sunsiro Sinza Dar es Salaam hivyo ametoa wito kwa wakazi wa vitongoji vya jirani kujitokeza kwa wingi.

“Ni jambo la kawaida kwa bendi kutoa burudani katika kila mkesha wa sikukuu yoyote hivyo mashabiki waje tusugue Kisigino ndani ya Sunsiro leo usiku” alisem Martin.

Aliongeza kwa kusema kuwa baada ya burudani hiyo kesho usiku, Jumatano usiku mpango mzima utahamia ndani ya ukumbi wa Club Bilicanas na baada ya hapo ratiba yao itaendelea kama kawaida ambapo siku ya Alhamisi watarudi Sunsiro kwa mara nyingine tena.

Hivi sasa bendi ya Twanga inatamba na albamu yake ya Mwana Dar es Salaam sambamba na mtondo na Sugua Kisigino.Kadhalika wana nyimbo mpya iliyotungwa na Saleh Kupaza ‘Mapenzi Hayana Kiapo’

Kalala Hamza Kalala 'Kalala Junior' na Khalid Chuma 'Chokoraa'.
Shhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh

Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh

Aisha Madinda

Post a Comment

0 Comments