Kampuni ya Vanedrick imeandaa mechi ya kumpongeza Rais wa Dkt. Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dkt. Ally Mohammed Shein pamoja na Wabunge wa vyama vyote vya siasa kwa kuchaguliwa kuingia bungeni.
Akizungumza jana na waandishi wa habari Mratibu Xavier Mhagama alisema kwamba medhi hiyo imepangwa kuchezwa Novemba 21 katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Mechi hiyo ambayo itapigwa kati ya timu mbili ambazo ni Dar es Salaam All Stars huku timu pinzani ikitokea kwa nyota wa Zanzibar.
Kocha wa timu ya nyota wa Dar es Salaam Jamhuri Kihwelu alisema kwamba timu yake itaingia kambini Jumatano ijayo katika hoteli ya Lamada iliyopo Ilala Dar es Salaam ambako watakaa hadi siku ya mechi.
Jamhuri alikija kikosi chake kuwa itaundwa na majina na timu wanazotoka kwenye mabano Ally Mustafa (Simba) na Ivo Mapunda (African Lyon) wote walinda mlango.
Freddy Mbuna (Yanga), Jabu Juma (Simba), Meshark Abel (African Lyon), Haruna Moshi Boban (Mchezaji Huru), Rashid Gumbo (Simba), Ibrahim Mwaipopo (Azam FC), Juma Seif (JKT Ruvu) na Salum Abubakar (Azam FC).
Wengine ni Monja Liseki (Mtibwa FC), Nsa Job (Yanga), Pius Kasambale (JKT Ruvu), Himid Mao (Azam FC), Amri Kiemba (Simba), Mohamed Kijuso (Simba), Mussa Mgosi (Simba), Jerson Tegete (Yanga), Adam Kingwande (African Lyon), Athuman Iddy Chuji (Yanga), Kelvin Yondani (Simba) , Kally Ongala (Azam FC), Salum Swedi (Azam FC) na Ramadhan Chombo a.k.a Ridondo (Azam FC).
Mara baada ya kutaja kikosi hicho Jamhuri amesisitiza kuwa Danny Mrwanda anayesakata kabumbu nchini Vietnam atatua nchini ili kuongeza nguvu huku timu ya Zanzibar wakitarajiwa kuwasili Novemba 19.
Meneja wa timu hiyo ni Mkurugenzi wa Kampuni ya MUZASHA , Muzamil Katunzi.
Mhadama alitaja viingilio katika mechi hiyo kuwa ni Jukwaa Kuu sh.10,000 Jukwaa la Kijani sh.8,000 na mzunguko ni sh.3,000.
MAKAMU WA RAIS KATIKA TUZO ZA RAIS ZA WAZALISHAJI BORA WA MWAKA
-
*Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango
akiwasili katika Ukumbi wa Super Dome uliyopo Masaki Jijini Dar es Salaam
kushiriki ...
8 minutes ago
0 Comments