Mkurugenzi wa Kampuni ya ASET, inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka akinadi CD ya Mapacha3. Anko Deo hakubaki nyuma alinyanyuka kwenye kiti na kuwatunza waimbaji, wacheza shoo na wapiga vyombo
Mapedeshee wanaopenda kumwaga mijihela kama kawa hapa naye alimwaga za kwake bila hesabu.
Aliyekuwa Msema Chochote MC Ben Kinyaiya hapa akiendesha Jahazi la Uzinduzi huo.
Mzee Yussuph alishindwa kujizuia kwa mlimbwende huyu akaanza kukamua naye taratiibu.
Mzee Yusuph akiimba sambamba na kundi hilo la Mapacha 3 wimbo waliomshirikisha wa Ushikapo Shikamana
Kama Kawaida yake Mfalme akitoa ghani zenye mguso katika Kibao cha Ushikapo na kusisitiza ushikacho ndicho chako na siyo cha mwenzako.
Hapa Jose Mara ambaye ni mmoja kati ya wasanii wanaounda kundi la Mapacha 3 akimkaribisha Mzee Yusuph
Mary ambaye pia ni rafiki wa karibu wa muimbaji Kalala Hamza 'Kalala Junior' akiikubalikazi ya bwana.
Mary akiendeleza makamuzi ya kumtunza Kalala Junior.
Rehema Kiluvia aliyenipa kisogo akimtunza Chokoraa.
Halima Kimwana furaha yake ilizidi kipimo Skin tight imechanika hajali kitu hapa ni burudani kwa kwenda mbele pia ni shabiki mkubwa wa chokoraa.
Hapa Halima akiwa katika hisia kali za muziki na wimbo aliokuwa akiimba Chokoraa.
Khalid Chuma 'Chokoraa' akionyesha umahiri wake wa kucheza, mbali ya kuimba na kurap.
Ikawa zamu ya Jose Mara mambo yaka mambo , hakika mapacha 3 ni zaidi ya vipaji.
Alivishwwa taji nayeye mashabiki wa Bongo Dar es Salaam wanamambo.
Hapa Jose Mara akionyesha utundu wake zaidi.
Mkongwe huyu Mafumu Bilal Bombenga naye aliwasapoti wasanii hawa hapa alikuwa akionyesha namna ya kucheza miondoko ya Mutwashii.
Kalala Junior naye Kiuno chake kilikuwa kivutio kikubwa usiku wa jana.
Kalala akiimba katika uzinduzi huo, ambapo pia kwa mujibu wao wamesema wazo la kuunda kundi hilo ni kutaka kujikwamua kimaisha nje ya bendi zao na mapato ya albamu watagawana sawa huku wakisimamia mauzo wao wenyewe.
Wacheza shoo waliovalia mavazi ya khanga hapa wakiwapa mgongo mashabiki na nyonga zao kama feni.
Kalala akiimba katika uzinduzi huo, ambapo pia kwa mujibu wao wamesema wazo la kuunda kundi hilo ni kutaka kujikwamua kimaisha nje ya bendi zao na mapato ya albamu watagawana sawa huku wakisimamia mauzo wao wenyewe.
Wacheza shoo waliovalia mavazi ya khanga hapa wakiwapa mgongo mashabiki na nyonga zao kama feni.
0 Comments