Vodacom Miss TZA kuondoka na Hyundai i10

Kampuni ya Vidacom Tanzania imetangaza zawadi za washindi wa shindano la kumsaka mrembo lililopangwa kufanyika Septemba 11, ndani ya ukumbi Mlimani City.Mshindi wa 1 atapata gari aina Hyundai i10 na kitita cha sh. mkilioni 8. Mshindi wa 2 atajishindia milioni 6 .2, wa 3 atapata milioni 4 na mshindi wa 4 atazawadiwa shilingi milioni 3 na wa 5 atapata shilingi milioni 2.4 wakati mshindi wa sita hadi wa 10 kila mmoja atapata shilingi mioni 1.4 watakaobaki watapata kifuta jasho cha sh 700,000 kila mmoja.
Baadhi ya warembo wakifuatilia michezo.
Kama ukipenda mambo ya utalii wa ndani wadau mnakumbuka Mbudya? Warembo wakikimbia na magunia katika fukwe ya Beach Eclipse
Ufukwe wa Eclipse kwa nje.
Hii ndiyo zawadi ya mrembo atakayetwaa tahi la Vodacom Miss Tanzania.Aina ya Hyundai i10 lenye thamani ya shilingi milioni 10 pia mshindi wa kwanza atapata na fedha taslimu kiasi cha sh.milioni 8.
Hili ni gari wanalotumia warembo kambini.
Mkuu wa Itifaki Kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye, Meneja Udhamini George Rwehumbiza wakiwa katika picha na baadhi ya washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010.
Washiriki wa shindano hilo wakiliangalia zawadi ya mshindi wa kwanza.
Wakishangilia gari mara baada ya kufunuliwa.
Hapa Hyundai bado haijafunuliwa Rwehumbiza akifafanua jambo.
Mwana Blog Dina Ismail akipozi mbele ya Hyundai i10 mtembelee http://www.mamapipiro.blogspot/.
Glory kutoka Vodacom, Grace Hoka Mhariri wa gazeti la Bingwa na Somoe (Nipashe) wakiwa nje ya Hoteli ya Giraffe View katika hafla hiyo.
Somoe akiwa na watoto mmoja wa ofisa wa Vodacom Nekta Foya.
Kanigusaaaaa. Mamapipiro, mimi mwenyewe kati na Amina (Majira).

Post a Comment

0 Comments