Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) Lord Sebastian Coe (kushoto) akipeana mkono na Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SHIRIKISHO la
mchezo wa Riadha Duniani (IAAF) limemteua Rais wa Shirikisho la Riadha nchini
(RT) Anthony Mtaka kuwa miongoni mwa wajumbe wanaounda kundi la ushauri wa
mikakati ya mawasiliano la shirikisho hilo.
Rais wa IAAAF ,Lord
Sebastian Coe alitangaza uteuzi huo hivi karibuni ambapo wajumbe wengine ni Abrahamson
Alan wa Marekani, Rodan Joe Junior ,Sierra Calixto
,,Karamarinov Dobromir kutoka Bulgaria na Rochdi Souad wa Ufaransa.
Akizungumza kuhusu
uteuzi huo Mtaka ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Simiyu alisema amepokea uteuzi
huo kwa furaha kutokana na kuwa ni nafasi ya juu katika sekta maarufu ya michezo katika
ngazi ya kimataifa.
“Nimefurahishwa na
uteuzi huu hasa ukizingatia nimeteuliwa nikiwa rais wa shirikisho la riadha mwenye
umri mdogo kuliko wote kwa sasa takuwa na fursa ya kujifunza mambo mengi
mazuri.”alisema Mtaka.
Alisema uteuzi huo
ni faida kubwa kwa maendeleo ya michezo katika taifa letu, hasa kipindi hiki
ambapo serikali ya awamu ya tano inapoandaa mkakati wa kuiweka sekta ya michezo
kuwa sehemu kubwa ya ajira.
Mtaka alisema Tanzania
itapata nafasi pana zaidi ya kuwakilishwa katika mikutano mikubwa ya mchezo wa
riadha duniani (Decision Making) eneo ambalo linatoa fursa kubwa kwa maandalizi
ya mashindano makubwa yajayo baada ya mashindano ya Olyimpiki yatakayofanyika
katika jiji la Rio de Jeneiro mwaka huu.
“Taifa litarajie
uwakilishi wenye tija, sababu mimi nimeteuliwa kati ya wajumbe nane ambao kila mmoja wao anawakilisha eneo kubwa,
hivyo kama nimepewa dhamana ya kuiwakilisha bara zima la Africa, kwa vyovyote
nitaweka maslahi ya nchi yangu mbele bila kuathiri utendaji wa jukumu
nililopewa.”alisema Mtaka.
“ Uteuzi wangu ni
sifa kwa taifa zima, sifa ambayo itafufua mtazamo mwema ulioonyeshwa na
wanariadha wakongwe walioiletea taifa sifa kama Filbert Bayi, Suleiman Nyambui,
Gidamis Shahanga, Juma Ikangaa bila kumsahau Mzee John Stephen Akhwari
aliyeshiriki Mexico City Games 1968.”aliongeza Mtaka.
Aidha Mtaka
alisema uteuzi huo umeongeza hamasa ya kuwekeza maradufu katika kambi ya timu
ya taifa ya riadha iliyopo katika hosteli ya Chuo cha misitu cha FITI kilichopo
West Kilimanjaro wilayani Siha na Arusha.
0 Comments