Social Icons

Tuesday, March 31, 2015

AIRTEL YAKARABATI DARASA SHULE YA MSINGI USHINDI


Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), akizungumza kabla ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), akimkabidhi Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni ‘B’, Suleiman Sagong’o, Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), akifungua mlango wa  Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni ‘B’, Suleiman Sagong’o na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), akiwasalimia watoto baada ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (mwenye miwani), na Afisa Mwandamizi wa Kitengo cha Biashara za Mashirika, Delfina Martin (mbele kulia), wakiwa wamekaa na watoto baada ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana.


Baadhi ya Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, wakigawa zawadi kwa watoto baada ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
 
DAR ES SALAAM

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa “Airtel Tunakujali”  wakishirikiana na wafanyakazi wa kitengo cha Airtel Biashara za Mashirika ameendeleza dhamira ya kusaidia jamii kwa kukarabati darasa la chekechea katika shule ya msingi Ushindi iliyopo jijini Dar Es Salaam. Leo Airtel imebadili mtazamo wa darasa hilo kwa kuwa jengo la kisasa na kuwapatia vitendea kazi  ikiwemo madawati na  michezo mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.

Shule ya Msingi Ushindi imekuwa miongoni mwa shule hapa nchini zilizoweza kuingia katika mfuko wa mradi wa  “Airtel Tunakujali” ili kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini. Baadhi ya shule ambazo zilishaweza kuingia  katika mradi huo ni Kumbukumbu Shule ya Msingi iliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam na shule ya Msingi Pongwe mjini Tanga. Lengo la mpango huu ni kuboresha mazingira ya wanafunzi na walimu mashuleni,kuwapataia wanafunzi elimu bora, kuhamasisha mahudhurio mazuri ya wanafunzi mashuleni na kunyanyua kiwango cha mfumo wa elimu katika katika taasisi hii.
Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano  , Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema, "Kutokana na dhamira ya Airtel tunafuraha kubwa sana kupata nafasi hii na kuwa ni wa moja wa makampuni yaliyopata nafasi ya kujenga mazingira bora na imara katika sekta ya elimu.  Leo hii tunakabidhi darasa zuri na la kisasa lenye Uwezo wa kukidhi idadi kubwa ya wanafunzi., hii itasaidia kupunguza shida iliyopo na kufanya mazingira ya kusomea kwa wanafunzi wengi kuwa rafiki. Tunaamini kwamba ubora wa elimu ni muhimu zaidi katika karne hii kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi hapa Tanzania. Sisi pia tunatambua changamoto nyingi katika ngazi zote za sekta hii muhimu.

Aliongeza " kwa kuboresha mazingira ya wanafunzi hawa ni kuchochea uelewa  na kuinua maisha yao ya hapo baadae. "Bila shaka, ubora wa elimu unawapa watoto nafasi bora katika maisha kutambua ndoto zao na kuwa viongozi bora wa kesho. Colaso aliendelea akisema, “anawaomba walimu na wanafunzi wa Ushindi watunze  rasilimali iliyotolewa kwao ili viweze kutumika na watoto wengine watakaokuja hapo baadae”.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi  ya Ushindi Elias Katunzi akitoa shukrani zake kwa Airtel alisema ,”kwa niaba ya walimu, wazazi na wanafunzi wa shule ya msingi ya Ushindi napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kuweza kututengenezea  darasa lililobora na imara . 

Ningependa kuwashukuru Airtel kwa yote waliyotufanyia kwa ajili ya shule hii. Kutokana na msaada huu tuanaamini kabisa idadi ya watoto itaongezeka kwani kwa sasa tunawatoto wapatao 50 wa chekechea.Tunaamini kwamba idadi ya watoto itaongezeka na wazazi watapata moyo zaidi wa  kuwaandikisha watoto wao hapa shuleni. Tunatarajia uandikishaji utaongezeka katika kipindi kitakachofwata "alibainisha Katunzi.

Mwalimu mkuu akaongeza pia kuwa anafurahi kwamba Airtel wameweza kuwasaidia katika tatizo hilo la ukarabati wa jengo na kuziomba taasisi  nyingine kuchangia sekta ya elimu katika shule mbalimbali kwani matatizo yanafanana nchini kote.

No comments:

 
 
Blogger Templates