Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Netiboli Mkoa wa Dar es Salaam (CHANEDA),kinatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wake Agosti 11, mwaka huu jijini.
Akizungumza na gazeti hili jijini jana, Ofisa Habari wa CHANEDA,Michael Maurus pichani kulia, alisema kuwa uchaguzi huo unafanyika, ikiwa ni baada ya viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wao tangu mwaka jana.
Alisema kuwa kuchelewa kufanyika kwa uchaguzi huo kulitokanana vyama vya wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke kutofanya chaguzi zao ilikupata wapiga kura halali ambao ndio watakaochagua viongozi wa mkoa.
“Ili uchaguzi ufanyike, lazima kuwapo na wapiga kura halali ambao ni viongozi wa klabu na vyama vya netiboli vya wilaya, tuliagiza vyamavifanye chaguzi, lakini hadi sasa hakuna mwitikio wowote, hivyo tumeonatuwatumie viongozi wa klabu kufanya uchaguzi huo wa mkoa ili viongoziwatakaopatikana wapange taratibu za kufuatilia kila chama cha wilaya kuona ninikinaendelea huko,” alisema Maurus.
Juu ya uchaguzi huo wa CHANEDA, Maurus alisema kuwamchakato wa uchukuaji fomu na kurudisha, unaanza Jumatatu ya Julai 23 hadi Julai 30, mwaka huu wakati usaili itakuwa ni Agosti 4, mwaka huu.
Maurus alisema kuwa fomu za kuwania uongozi huozinapatikana katika ofisi ya Ofisa Michezo Mkoa wa
Dar es Salaam.
Kwa sasa viongozi waliobaki wanaokisimamia chama hicho niMwenyekiti Winfida Emmanuel, Katibu Mkuu Joseph Ng’anza na Maurus akiwa kamaOfisa Habari na Katibu Msaidizi.
Wengine waliokuwa na nafasi CHANEDA ambao hata hivyohawakuwa karibu na chama hicho kutokana na sababu mbalimbali, ni Jackson Henzron(Mweka Hazina), Christina Kimamla, Mussa Sambala, Khadija Ally na Moshi Mganga (wotewajumbe), huku Makamu Mwenyekiti akiwa ni Pili Mogella ambaye hata hivyo alijiondoakutokana na kutohudhuria vikao.
0 Comments