TUSKER MALT LAGER YADHAMINI TAFRIJA YA HISANI YA SHEAR KIASI CHA SH. MIL25

TUSKER  MALT LAGER YADHAMINI  TAFRIJA YA HISANI YA SHEAR
(Shear Charity Ball 2011)YENYE LENGO  LA KUSAIDIA  MRADI WA FISTULA  KATIKA HOSPITALI YA CCBRT NA PIA  KUWEZESHA KUKARABATI MFUMO WA MAJI KATIKA HOSPITALI YA AMANA
 Kutoka kulia  ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ShearIllusions Shekha Nasser ambaye pia  ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tafrija ya Shear Charity Ball 2011, katikati ni Ofisa wa Mahusiano ya Jamii Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Nandi Mwiyombela na Ofisa wa Idara ya Mambo ya Ndani SBL Imani Lwinga wakizungumza na waandishi leo asubuhi katika ofisi zao zilizopo Oysterbay Dar es Salaam.
  KAMPUNI ya Bia ya Serengeti imetangaza kutoa udhamini mnono kwa katika kuchangia na kufanikisha tafrija ya ‘Shear Charity Ball 2011’ itakayofanyika Jumamosi Oktoba mosi katika hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam.
Akitangaza udhamini huo Meneja wa Mahusiano ya Jamii Kampuni ya Bia Serengeti Nandi Mwiyombela alisema.
“Kampuni ya Bia Serengeti ambao ndiyo wadhamini wakuu tuna kila sababu ya jivunia kutangaza kuwa tumechangia kiasi cha sh. mil 25 katika kufanikisha tafrija hii ambayo itaenda sambamba na chakula cha usiku pamoja muziki” alisema .
Alisema tafrija hii itaanza saa moja kamili jioni
Huku wageni walikwa wakiwa wametakiwa kuvaa katika mavazi yenye rangi nyeupe na nyeusi.
“Katika tafrija ya mwaka huu ambayo inafanyika kwa mara ya pili sasa imelenga kuchangisha kiasi cha sh.mil 50 kwa ajili ya taasisi mbili ambazo ni CCBRT na Hospitali ya Amana”alisema Mwiyombela.

Wakati huohuo Mwiyombela aliongeza kwa kusema kuwa leo wasanii wa kundi la Mutati kutoka nchini Kenya watawasili nchini ambapo watatoa burudani katika tafrija hiyo.

“Kesho usiku kutakuwa na muziki katika ukumbi wa Nyumbani Lounge na kiingilio kitakuwa sh.10,000 napenda kuwaeleza kwamba fedha hizo zitapelekwa katika kuchangia matibabu ya upasuaji kwa wagonjwa wa Fistula katika hospitali ya CCBRT na kuweka mfumo wa maji safi na taka Amana
” alisema .

Kulia ni Mwandishi Mwandamizi kutoka gazeti la The African Mwani Nyangassa 'Wifie' linalochapishwa na Kampuni ya New Habari akiwa makini katika kuchukua maelezo katika mkutano huo. 
KWA MHARIRI:
Serengeti  Breweries kwa kupitia  mipango  ya uhusiano wa jamii inayozunguka  Tanzania tunajivunia  miradi mbalimbali  inayosaidia  watu waweze kujisaidia.
SBLimejikita  kwenye  sehemu muhimu :maji stadi za maisha , afya na mazingira.Kipaumbele  ni kusaidia kwenye  miradi  endelevu ya maji safi kwa jamii yetu.
Pia tunamiradi  mingine  Tanzania ya kukumbuka kama kliniki ya macho mjini Moshi ambayo imejengwa  na SBLna inasaidia  mamilioni ya watu mkoani  hapo.
Mradi mwingine  ni ufadhili wa masomo ya juu kwa wanafunzi waliofaulu vizuri  ila hawana uwezo  kujiunga  na chuo  kikuu .Hii ni kutoka  mfuko wa EABL Foundation  Scholarship programme.Mpaka sasa mfuko huo umesaidia  wanafunzi  zaidi  ya 160 wakiwemo 20 kutoka Tanzania.Waliojipatia  fursa  ya kusomeshwa  kwa miaka sita  iliyopita wamejiunga  na chuo kikuu cha Dar es Salaam, na chuo  kikuu cha Mzumbe.Kwa mwaka  huu  tumetengaza  tena ufadhili na wanafunzi waliopita  vizuri  na wana nia  ya kuendeleza masomo  yao kwenye  vyuo vikuu nchini wanakumbushwa kujaza fomu za kuomba ufadhili

Post a Comment

0 Comments