WADAU NIMERUDI TENA D'SALAAM BAADA YA KUWA KATIKA MAPUMZIKO MAFUPI MKOANI DODOMA

Hapa nikiwa katika moja ya mapumziko yangu mwishoni mwa wiki iliyopita , katika mapumziko yangu Mkoani Dodoma niliweza kuwatembelea ndugu na jamaa hapa nikiwa katikati ya bibi na babu yangu bwana na bibi Hedtjarn ambaye ni Mkurugenzi wa Tanzania Photomap Limited wanaoishi Maeneo ya Maili mbili.
Mjukuu hakui eti na raha yake eti kama mnavyoona hapa shangazi yake baba bibi akinitazama kwa huba zito , hakika nimefurahia safari yangu na Mji wa Dodoma umetulia kwa kweli.

Wadau nimerudi tena Jijini Dar es Salaam baada ya kupigwa na kipupwe cha Mkoani Dodoma nilikokwenda kwa mapumziko mafupi mwishoni mwa juma ambapo nilikwenda kupumzisha akili na mwili Habari zenu bana hapa nikiwa niko nje ya usafiri wetu wa ukweli .

Kutoka kushoto ni JKmdau mkuu wa Blog hii , mimi Khadija na George ambaye hivi sasa anafanya kazi katika Kampuni ya Intergrated Communications Limited Dar es Salaam.Hapa tukiwa katika moja ya kiota cha kuvutia yaani ni kipya hata jina hakina kilichopo Gairo.
Vijana wa zamani wa Area C , Dodoma JK na G. Muhina walipokutana hapa wakibadilishana mawazo safarini na kukumbushana mastori ya miaka kibao iliyopita.

Nikipozi kwa picha .


Kutoka kushoto Mdau mkubwa wa blogu hii JK, mimi Khadija 'Lindashebby' na mdau mwingine.

Wadau hapa ni Gairo ambako kuna kiota hiki kipya tulishuka muda mfupi na kupata mlo kila kitu kinapatikana hapa yaani hii ilikuwa ni safari ya mapumziko mafupi Mkoani Dodoma.

Post a Comment

0 Comments