Na Mwandishi Wetu
MICHUANO ya Ester Cup inayofadhiliwa na mbunge wa viti maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ester Bulaya, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo wilayani Bunda mkoani Mara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jijini Dar es Salaam, mbunge huyo alisema lengo la mashindano hayo ni kukuza vipaji, kutoa burudani pamoja na kuwakutanisha vijana pamoja ili kukuza umoja na mshikamano baina yao.Alisema mashindano hayo yatazishirikisha timu 10 zitakazopepetana katika viwanja vya Sabasaba na Shule ya Msingi Bunda ambapo kilele chake kitakuwa Mei 4 mwaka huu.Aidha Bulaya alibainisha kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia seti ya jezi, kombe na mipira miwili, mshindi wa pili atajitwalia seti ya jezi na mpira mmoja huku mshindi wa tatu atakabidhiwa seti ya jezi.Timu yenye nidhamu itakabidhiwa seti ya jezi huku mfungaji na golikipa bora kila mmoja atajinyakulia mpira mmoja.
“Nimedhamiria kuwaunganisha vijana pamoja kwa kuwa ubunge wangu niliupata kwa tiketi ya vijana, nina mpango wa kugawa jezi, mipira na viatu katika Kata zote za mkoa wa Mara,” alisema Bulaya.Alisema anaamini kuwa michezo ni ajira hivyo wataitumia michuano hiyo kuonyesha vipaji vyao vitakavyowawezesha kuonekana kwa wadau ili wasajiliwe katika klabu mbalimbali.

0 Comments