Waandishi wa habari 11 wamepongezwa kwa kujitokeza kwa wingi kukata bima za maisha na mali katika maonesho ya nanenane yanayofikia kilele leo tarehe 8 Agosti 2026 Jijini Dodoma, hatua iliyoelezwa kuwa ni mfano bora kwa wananchi katika kujenga utamaduni wa kujilinda dhidi ya majanga mbalimbali.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Shirika la Bima la Taifa (NIC Insurance), Karimu Meshack, amesema waandishi wa habari wameonyesha uelewa mkubwa kwa kuamua kutekeleza kile ambacho kwa muda mrefu wamekuwa wakikihamasisha kwa jamii kupitia kazi zao.
Meshack amesema ndani ya siku moja pekee waandishi wa habari 11 walikata bima za maisha na mali, jambo alilosema linaonyesha mabadiliko makubwa ya mtazamo kuhusu umuhimu wa bima kwa watu wanaofanya kazi zenye mazingira yenye hatari na changamoto mbalimbali.
Alisema kuwa waandishi wa habari ni daraja muhimu la kuwafikishia wananchi elimu ya bima, hivyo uamuzi wao wa kujiwekea kinga ya kifedha unawapa nguvu ya kuzungumza kwa uzoefu na kuwa mfano wa kuigwa na makundi mengine ya jamii.
Aidha amamewahimiza Waandishi wengine kote nchini kuufuata mfano huo kwa kutambua kuwa, pamoja na taaluma yao ya kuhabarisha umma, wao pia ni wazazi, walezi na wategemezi wa familia wanaohitaji ulinzi wa maisha na mali zao.
Baadhi ya Waandishi ambao ni Tatu Mohamed na Sofia Kingimali waliokata bima ya maisha huku Khadija Kalili alikata Bima ya nyumba wote kwa pamoja walisema wameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha familia na mali zao zinakuwa salama endapo yatatokea majanga yasiyotarajiwa.
Meshack amesema ongezeko la waandishi wawanaokata Bima linaunga mkono jitihada za Serikali za kuongeza ushiriki wa wananchi katika huduma za Bima pia amesisitiza kuwa kulinda maisha na mali ni msingi wa kulinda uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
Ametoa wito kwa wananchi wote kuiga mfano wa Waandishi wa habari 11 kwa kujitokeza kukata Bima mbalimbali kulingana na mahitaji yao, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kujenga jamii yenye usalama wa kifedha na kuongeza ustahimilivu dhidi ya majanga yasiyotarajiwa.
Aidha Khadija amesema kuwa alipata msukumo wa kukata Bima ya Nyumba baada ya kuona watu wake wa karibu waliokumbwa na majanga ya kuunguliwa nyumba wakikosa fidia kutokana ukosefu wa elimu ya kuweka ulinzi katika mali zao na kuahidi kuwa Balozi wakutoa elimu ya umuhimu wa kukata Bima kwa Waandishi wengine pamoja na jamii nzima kwa ujumla kwa sababu hakuna anayeijua kesho nini kitatokea.
Wakati huohuo Afisa Uhusiano na Mawasiliano TIRA Anna Massao amewakaribisha wananchi kufika katika banda lao kupata elimu ya Bima amesema tuko hapa kutoa elimu pia majukumu yetu ni kuandaa kusajili kutoa leseni kwa wote wanaotoa huduma za Bima lakini pia tunajukumu la kuandaa miongozo inayotoa kanuni na Bima .
Msuluhishi Mkuu kutoka ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Aloyce Mbunito amesema kazi kubwa ya ofisi hii ni kusuluhisha migogoro ya Bima kwa njia mbadala ya Mahakama ili kupata fidia kuna watu wanapata majanga na wengi wameshindwa kupata suluhu ya majanga yao ikiwa kupunjwa kuzngushwa au kupata mafao ya chini.
.

0 Comments