MHE.ASHA BARAKA,ALLY CHOKI,MANGUNGU WASIKITISHWA NA KIFO CHA EMMANUEL MACHA

 
 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani  kupitia   Chama Cha Mapinduzi (CCM) 
Asha Baraka  jana alikua miongoni mwa watu mashuhuri  waliojitokeza kwenye mazishi ya Emmanuel Nderimo almaarufu Macha Magari  ampapo ameeeleza kwamba ameguswa na kusikitishwa sana na msiba huo mzito kwani marehemu kwa upande wake alikuwa ni mmoja ya mtu muhimu sana katika kuleta chachu ya maendeleo katika  muziki wa dansi pamoja na mchezo wa soka ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wake kwa kusaidia  mtu mmoja mmoja  hivyo marehemu ameacha pengo kubwa sana.

Naye muimbaji  maarufu wa muziki wa dansi hapa nchini Camarade  Ally Choki alikua miongoni  mwa wasanii walihudhulia katika msiba huo  katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya Kinondoni  Jijini  Dar es Salaam.


Na  Mwandishi  Wettu ,Dar 

 Viongozi wa serikali, viongozi wa dini, taasisi na mashirika binafsi ,mashabiki wa soka na muziki wa dansi  na mamia ya wananchi  mbali mbali  wamejitokeza kwa wingi katika mazishi ya Emmanuel Nderimo  Macha Magari  yalitofanyika tarehe  01 Aprili 2026 katika kaburi ya Kinonddoni Jijini Dar es Salaam.

 
Katika enzi za uhai wake   marehhemu Macha alikua ni mfanyabiashara maarufu  wa kuuza magari pia alikua shabiki mkubwa wa Klabu ya soka ya Simba ,Nderimo  amefariki dunia Machi30  2026.

Katika mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na chama cha mapinduzi (CCM) yalikubikwa na vilio na majonzi makubwa ambayo yalipelekea baadhi ya watu kushindwa kujizuia kwa kutokwa na machozi wakati wa zoezi la kuuga mwili huo.

Moja kati ya viongozi maarufu ambao walihudhulia katika msiba huo ni Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba Murtaza Mangungu pamoja ambapo aliambatana na viongozi wengine mbali mbali wa klabu hiyo ambapo amesema marehemu Emmanuel alikuwa na mchango mkubwa sana katika klabu hiyo kwani alikuwa mstari wa mbela katika kusaidia mambo mbali mbali

 Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro naye alikuwa ni mmoja wa viongozi wa ulinzi na usalama ambaye naye alifika kwa ajili ya kutoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Emmaanuel Nderimo.


 
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe,Silvestry Koka ambaye marehemu ni shemeji yake hakusita kumwelezea marehemu jinsi alivyokuwa ni mpambanaji katika mambo mbali nmbali na kwamba alikuwa ni mtu wa kusamehe sana pindi unapomkosea na kwamba alikuwa ni mstari wa mbele katika kutoa ushauri wenye kujenga.

"Kwa kweli mimi nimesimama hapa kwannza kabisa namshukuru mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kutukutanisha hapa katika msiba wa ndugu yetu Emmanuel lakini kitu ambacho nataka kukisema inapaswa tuishi kwa kupendana sana na ndio maana marehemu alikuwa na upendo mkubwa sana na watu mbali mbali na alikuwa ni mwepesi sana katika suala la kusamehe kwa hivyo inapaswa tujifunze mazuri ambayo ametuachia."amebainisha Mhe. Koka.

Nao baadhi ya viongozi na mashabiki akiwemo Mama Asha Baraka ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) amesema kwamba ameguswa na kusikitishwa sana na msiba huo mzito kwani marehemu kwa upande wake alikuwa ni moja ya mtu muhimu sana katika kuleta chachu ya maendeleo katika ttimu pamoja na kuweza kusaidia mtu mmoja mmoja kwa hivyo ni pengo kubwa sana ambalo ameliacha.

Post a Comment

0 Comments