WANAFUNZI WA MADRASA ,WAALIMU KUTOKA KONDOA WATHIBITISHA KWA MUNGU HAKUNA KUBWA NGORONGORO



Mwenyezi Mungu akitaka jambo litokee hutokea ndivyo ilivyotokea, uumbwaji wa Kasoko ya Ngorongoro zaidi ya miaka milioni 2.5 iliyopita ambapo mlima mrefu uligeuzwa kuwa bonde la Ngorongoro.

Wanafunzi wa madrasa kutoka jimbo la Kondoa mkoani Dodoma pamoja na walimu wao wameshuhudia uwezo huo wa Mwenyezi Mungu walipotembelea hifadhi ya Ngorongoro katika ziara iliyoandaliwa na mbunge wa jimbo hilo mheshimiwa Dkt Ashatu Kijaji (Mb)

Afisa Mhifadhi Mkuu na mkuu wa makumbusho ya Urithi Geopark Dkt. Agnes Gidna aliwaeleza wanafunzi na waalimu hao kuwa mlipuko mkubwa wa volcano uliugeuza mlima mkubwa uliokuwepo eneo hilo zaidi ya miaka milioni 2.5 iliyopita na kuwa kreta hii ni kudhihirisha wazi kwamba kwa Mungu hakuna jitihada 

Akizungumza kwa niaba ya kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka hiyo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Gloria Bideberi amempongeza mbunge wa jimbo hilo Dkt. Ashatu Kijaji ambaye pia ni waziri wa maliasili na Utalii kwa kusimamia sekta hiyo kwa vitendo ambapo ujio wa wanafunzi hao utaongeza jitihada za kutangaza utalii wa ndani.

Kiongozi wa Ujumbe huo Katibu wa Idara ya Elimu ofisi ya mbunge wa jimbo la Kondoa Ayoub Sogoi amesema ziara hiyo imedhihirisha kwa vitendo mafunzo wanayopata vijana hao kutoka madrasa na shule za msingi na sekondari.

Post a Comment

0 Comments