MTANZANIA AULA M4FOFA

 

Mtanzania ameteuliwa  kuwa Mjumbe wa Bodi ya  Shirika la The Movement for the Federation of East Africa (M4FOEA)

Shirika hili ni Muunganiko wa nchinane za Jumuiya ya Africa mashariki  ambazo ni Uganda ,Kenya ,Somalia , Rwanda ,Burundi , Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),Sudani Kusini na Tanzania.

Malengo ya Shirika hilo ni kuhakikisha linazalisha vijana wazalendo wenye uwezo  wa 
kulinda amani ya bara la  Afrika, Kutetea haki na usawa kwa ajili ustawi wa Afrika, kuzipenda nchi zao,kulinda na kuenzi tunu za waasisi wa mataifa hayo.

Mchakato wa kuwapata wajumbe wa Bodi ulianza tarehe 10 Januari 2026 baada ya Shirika hilo kutangaza nafasi hizo. 

usaili na vikao vya uteuzi vimechukua zaidi ya miezi mitatu katika mchakato wa  kuwapata watu makini watakaolitumikia Shirika hilo.

Shirika hilo ambalo Makao Makuu yapo nchini Uganda na Mlezi wake ni  Rais  Yoweri  Kaguta Museveni  wa Uganda.

 Akizungumza  baada ya uteuzi huo Punzi  ameshukuru  nchi yake ya Tanzania na Kamati nzima ya ufatiliaji maana siyo jambo jepesi kuvuka hatua hizo ngumu pia amewaomba vijana kujiunga katika Shirika hilo ili kuwa sehemu ya kuenzi na kulinda amani yetu

Post a Comment

0 Comments