Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Pwani Edson Mwakihaba amesema kua barabara hizo chepuzi zimesaidia katika kupunguza msongamano wa magari ," kwa sababu ajali zilizokua zikitokea husababishwa na mwendo kasi wa magari huku barabara hiyo ya Morogoro hairuhusu gari kwenda kasi kutokana na wembamba wa bababara na wingi wa magari" amesema RTO Mwakihaba.
Wakala wa Barabara TANROADS Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani wameruhusu mchepuko wa Barabara kuanzia maeneo ya Kibaha Mailimoja hadi Mlandizi Wilayani Kibaha kwa lengo la kumaliza foleni za magari kuanzia maeneo ya mailmoja zilipoishia Barabara nane za kutokea jijini Dar Es salaam.
Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Pwani Baraka Mwambage akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Kibaha amesema kuwa barabara hiyo ya mchepuko itasaidia kupunguza ajali za barabarani zinazotoka na madereva wa magari kulazimika na kushawishika kuendesha kwa mwendo kasi ili kuzipita magari mengine (Overtaking) wakati barabara hairihusu kutokana na wingi wa magari.
"Barabara hii ambayo tumeichepusha inaanzia Kibaha Mailimoja hadi Stendi ya mabasi yaendayo Mikoani na baada ya hapo itaendelea kutoka Picha ya Ndege hadi Msufini Mlandizi na ambayo iko katika kiwango cha changarawe" amesema Meneja Baraka.
"Wakati serikali inaendelea na utekelezaji wa mkakati wa ujenzi wa barabara harakishi kati ya Kibaha Mailimoja njia ya Morogoro kupitia Chalinze TANROADS Pwani imejipanga kufanya ukarabati wa barabara ya zamani iliyopo barabara ya Morogoro kwa upande wa Mkoa wa Pwani yenye urefu wa Kilomita 66.11”.
Meneja Eng.Mwambange amesema serikali inampango wa kuongeza Barabara moja kila upande kuanzia eneo la Mailmoja
Wilayani Kibaha hadi maeneo ya Ubena Zomozi.
“Mkakati mwingine wa muda mfupi ambao utakuwa ni wa pili wa kuendeleza jitihada za kumaliza foleni za magari ni pamoja na kujenga Barabara za lami pembezoni mwa Barabara zilizopo kila upande ndani ya hifadhi ya barabara mpaka
Ubena Zomozi kisha hadi Mkoani Morogoro” amesema Eng. Baraka.
Amesema kuwa mpango huo wa kupunguza msongamano wa magari kwa kuboresha barabara ya Morogoro TANZAM inayoanzia Dar es Salaam hadi Tunduma mpakani na nchi ya Zambia ambayo ni lango kuu la usafiri na usafirishaji kwenda Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ni endelevu.
Eng. Baraka amezitaja nchi zinazonufaika na matumizi ya Barabara hiyo kuwa ni Pamoja na nchi za Kaskazini na nchi jirani kama Zambia , Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Madereva wa magari makubwa , waenda Bodaboda wameshkuru TANROAD Mkoa wa Pwani kwa kuwatatulia tatizo la foleni ya magari barabarani kwa kutenga barabara ya mchepuko kutoka Kibaha Mailimoja hadi
Dereva Kassim Mohammed Kassim ambaye anaendesha gari kubwa ametoa pongezi kwa serikali kuja nanuamuzi huo wa kuweka barabara ya mchepuko inayotoka Kibaha Mailimoja hadi Msufini Mlandizi kwa kuwa imepunguza msongamano.
"Tunashkuru kwa kuwekewa barabara hii
'By Pass' kutoka hapa Kibaha Mailimoja hadi Stendi ya Mabasi ya Mkoani na baada ya hapo inaendelea Picha ya Ndege hadi Msufini Mlandizi imetusaidia sana" amesema Dereva Kassim.
Hapa ndipo inapoanza barabara chepuzi .Alama imewekwa ikionesha gari zinazoruhusiwa ni zile zinazotoka Mlandizi na Chalinze Mkoa wa Pwani kwenda Jijini Dar es Salaam.









0 Comments