Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kulea na kuwawezesha waandishi wa habari wa mitandaoni na mabloga, badala ya kuwashughulikia kwa mtazamo wa adhabu, ili kujenga tasnia imara na yenye tija ya habari nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18 Desemba 2025 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, ameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mwelekeo wake wa kulea wadau wa sekta ya habari badala ya kuchukua hatua kali za kinidhamu.
Msigwa amesema kuwa mwelekeo huo unaendana na falsafa ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambayo inalenga kushirikiana na wadau mbalimbali kwa manufaa ya taifa.
" Tanzania Bloggers Network (TBN) na Jukwaa la Mitandao Tanzania (JUMIKITA) kuwa ni wadau wakubwa wa serikali katika tasnia ya habari, mchango wao ni muhimu katika kusambaza taarifa na kujenga mawasiliano kati ya serikali na wananchi." amesema Msigwa.
“Serikali inawaamini Waandishi wa mitandaoni, sasa nanyi muendelee kuonesha imani kwa serikali. Ushirikiano wetu umeendelea kuimarika na changamoto zinazojitokeza tunazitatua kwa pamoja,” amsema Msigwa.
Aidha Msemaji wa Seeikali amekanisha vikali madai kuwa Waandishi wa Habari wa mitandaoni kuwa ni dhaifu, Msigwa amesema wanatekeleza wajibu wao ipasavyo na wana nafasi kubwa ya kutumia kalamu zao kujengakatika kujenga taifa.
“Nimekuwa nikisisitiza Waandishi tutumie kalamu zetu kujenga nchi.mnafanya kazi sahihi na mnalinda maslahi ya taifa,” amesema Msigwa.
" Ukitazama sera zao wao zinaruhusu mambo ambayo kwetu, kitaifa, kijamii na kwa usalama wa nchi yetu hayatakiwi kisheria, basi ndiyo hulazimika kufunga tu, lakini tukijua athari zake kiuchumi hasa ninyi mnaotumia mitandao hiyo kuingiza kipato" amesisitiza Dkt Jabiri.
Msigwa amewahakikishia Waandishi wa Habari Mmitandaoni ulinzi wa serikali huku akisema endapo sheria, kanuni au sera zitabainika kuwa kikwazo katika utendaji wao, zitafanyiwa marekebisho kwa maslahi mapana ya taifa.
Ametngaza pia kuanza kwa maandalizi ya mafunzo kwa waandishi wa habari kwa kushirikiana na TCRA, akiwataka kuyapokea kwa mtazamo chanya kama sehemu ya kuongeza weledi na taaluma.
Kuhusu masuala ya kodi, Msigwa amesema serikali itaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kutatua changamoto zinazowakabili Waandishi wa Mitandaoni huku amebainisha kuwa anatambua mchango wao katika kuitangaza nchi na kuvutia uwekezaji.
Aidha,almeeleza kuwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ipo katika mchakato wa kuanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya kuwawezesha Waandishi wa habari, hususan wa mitandaoni.
Akizungumzia mazingira ya ssasa za kimataifa, Msigwa amesema vita vya dunia ya sasa imehama kutoka silaha za kijeshi kwenda kwenye upotoshaji wa taarifa , amesema kuwa vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kulinda na kutangaza mema ya nchi.
Amewahimiza Waandishi wa Haabari za Mtandaoni kuwa majukwaa yao yanattumika kulinda maslahi ya taifa na kuonya dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao yanayoweza kuharibu taswira ya Tanzania.
Hata hivyo, Msigwa amesema kuwa kusikitishwa na tabia ya baadhi ya waandishi kunyamaza wanapodhalilishwa, akiwataka kusimama na kulinda hadhi ya taaluma yao.
" Hivi karibuni Waandishi wa Haabari wa Tanzania mmeitwa waoga jibuni mapigo hivi kweli mnashindwa kujitetea kwa kutoa matamko ili Dunia iwasikie msiishi kinyonge wala msikubali kuwa wanyonge toeni matamko dunia iwasikie" amesema Msigwa.





0 Comments