WASANII WA KIMATAIFA KUNOGESHA TUKUTANE DAR ARTS WEEK

Mkurugenzi wa Nafasi Art Space Lilian Hypolite  akizungumza  na Waandishi wa habari hawapo pichani leo tarehe 24 Novemba  ,2025 Jijini Dar es  Salaam. 


Na Mwandishi Wetu, Dar

Wasanii nyota duniani na wa Kimataifa kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika wanatarajiwa kupamba onesho hilo.

Aidha wasanii na wadau zaidi ya 3,000 kutoka nchi mbalimbali za Afrika na mataifa mengine duniani wanatarajiwa kushiriki katika tamasha la ‘Tukutane Dar Arts Week’ linaloandaliwa na Taasisi ya Nafasi Art Space ya hapa nchini.

Tamasha hilo limeanza rasmi leo, Novemba 24, 2025 litarindima hadi Novemba 30, mwaka huu mwaka huu.

 Akizungumza na Waandishi wa habari katika mkutano ulliofanyika Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Nafasi Art Space Lilian Hypolite amesema kuwa 

Tamasha hilo litawakutanisha wasanii, wasimamizi wa sanaa na utamaduni, wanafunzi wa masuala ya sanaa pamoja na wadau wa sekta kwenye hiyo kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kujifunza na kuimarisha ushirikiano.

 Hipolyte, amesema kuwa huu ni msimu wa tatu tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo la muziki.

Mkurugenzi huyo ameongeza kwa kusema kuwa mataifa yanayotarajiwa kushiriki ni pamoja na Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) , Rwanda, Kenya, Uganda, Ujerumani, Poland na Canada.

 "Wasanii wengine wanaotarajiwa kuonesha vipaji vyao ni kutoka Mikoa ya Dodoma, Mtwara , Mwanza na Zanzibar"amesema Hipolyte. 

Amefafanua kuwa wadau hao wakiwa katika kongamano hilo la muda wa wiki moja watapata muda wa kutafakari, kubadilishana mawazo, kupata mafunzo na kubuni mbinu mpya za kuimarisha mfumo wa sanaa na utamaduni barani Afrika.

Mkurugenzi Mkuu wa Nafasi Art Hipolyte amesema kuwa 

Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Ushirikiano wa Kikanda kwa Maendeleo ya Sekta ya Utamaduni na Ubunifu (CCI)’ ikilenga kuhimiza umuhimu wa ushirikiano wa Kikanda katika kukuza sekta ya ubunifu na utamaduni.

Aidha amesema kuwa tamasha la mwaka huu meongeza kuwa tamasha la mwaka huu litafanyika katika maeneo saba makuu ya sanaa na utamaduni Jijini Dar es Salaam ambayo ni Nafasi Art Space, Goethe-Institute, CDEA (Culture and Development East Africa), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Ajabu Ajabu, Tai Studio pamoja na Muda Kona.

“Tamasha litakuwa na ratiba yenye matukio mbalimbali makubwa yakiwemo warsha, madarasa maalum, mijadala ya paneli, maonyesho ya sanaa, uoneshaji wa filamu, maonesho ya kazi za wasanii pamoja na shughuli za ustawi wa mwili na akili,” amesema Hipolyte.

Wasanii wengine walioalikwa ni wasanii wasimamizi wa kazi za sanaa, watendaji wa sekta ya utamaduni na wadau wa ubunifu kushiriki tamasha hilo ili kukuza ubunifu, kuongeza maarifa na kuimarisha ushirikiano katika sekta hiyo.

Wakati huohuo Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Abel Ndaga akizungumza katika mkutano huo waandishi wa habari amesema jukwaa hilo litasaidia kujenga uwezo wa wasanii na kuwapanua mbinu za mauzo ya kazi zao na amesisitiza kuwa sanaa inaendelea kukua nchini kwa sababu sanaa ni ajira na biashara ya kudumu.

"Wasanii wanajiingizia kipato kwa kupitia kazi zao, kinachowasaidia kujikwamua kiuchumi na kuchangia ukuaji wa uchumi wa pato la taifa kwa kulipa kodi,” amesema Ndaga.



 Aidha Mtengenezaji wa filamu na Mwanzilishi wa Kampuni ya TAI Studio, Gwamaka Mwabuka, amesema tamasha hilo limekuwa fursa muhimu kwa wasanii kufungua milango ya ushirikiano na wabunifu kutoka mataifa mengine.

“Nilipohudhuria maonesho mbalimbali nje ya nchi, nimekutana na msanii mmoja wa kike aliyebobea katika utengenezaji wa vikaragosi.

 "Msanii huyo ameonesha nia ya kuja nchini , hivyo nimempa mwaliko na atamuwepo kwenye tamasha hili

, ambapo atawapa wasanii elimu na uzoefu wake,” amesema.

Post a Comment

0 Comments