SMAUJATA MOROGORO YAWAASA VIJANA



Na Mwandishi Wetu,Morogoro 
Mwenyekiti SMAUJATA Mkoa wa Morogoro Joyce Hamisi Nyangi amewaasa wahitimu kujiepusha na vitendo viovu katika jamii.

Nyangi amesema hayo aliposhiriki katika mahafali ya Kidini Chuo Cha FDC ILONGA ya CASFETA na Ukwata.


 Nyangi ambaye alikua ndiyo mgeni rasmi kwenye mahafali hayo amewaeleza wahitimu hao kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa kuelezea maana ya ukatili na jinsi ya kuepuka vitendo vya ukatili na pia kuwaasa vijana kuilinda amani ya nchi ambayo ni tunu ya taifa.

" Endapo utapata taarifa za ukatili toa taarifa kwa vyombo husika endapo wanaona viashiria vya kuvunjika amani" amesema Nyangi.

Akiwa kwenye mahafali hayo amewaambia daima waendeleze kauli mbiu isemayo kataa ukatili wewe ni shujaa.

Post a Comment

0 Comments