Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Mbunge wa Makunduchi Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Wanu Hafidh Ameir anastahili uWaziri kamili na sio uNaibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alioteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hivi karibuni.
Akizungumza na Wanahabari, CCM Kisiwandui 19 Oktoba 2025, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Taifa, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema kuwa uzoefu wake Baraza la Wawakilishi na ushindi wake wa kishindo jimboni Makunduchi vinambeba.
"Kama Mheshimiwa Rais angetaka ushauri kwangu mwenezi wa CCM huku Zanzibar ningemwambia ampe uWaziri kamili" alisema Mbeto.
Alibainisha kuwa Wanu, Rais hakumteua kwenye nafasi zake 10 wala hayupo Bungeni kwa Viti Maalum, alisimama jimboni Makunduchi na akashinda kwa kishindo hivyo haoni kama wanaohoji uWaziri wake kama wana hoja.
"Rais anapoteua maWaziri anaangalia vitu vingi ikiwa ni pamoja na uwiano wa nchi na sifa mojawapo ili uwe mbunge ujue kusoma na kuandika na Wanu uzoefu anao amekuwa Viti Maalum katika Baraza la Wawakilishi kwa miaka chungu nzima, kosa lake lipi? Au kwa kuwa mama yake Rais?" alihoji Mbeto.
Mbeto alisema kuwa hakuna chuo kinachofundisha uWaziri na kuteuliwa katika nafasi hiyo lazima uwe na sifa ya kuwa Mbunge na sio vinginevyo.
"Wanu kapambana jimboni na mama yake (Rais Samia), hakuwepo huko na ni wanawake wachache wanaomudu kusimama majimboni, kwanini tusimpongeze?" alisema Mbeto.
Mwenezi Mbeto alisema kupitia Umoja wa Wanawake CCM (UWT), angetaka viti maalum asingekosa lakini kaamua kupambana jimboni.
"Nashangaa wanaohoji, Rais Samia hakukosea kumteua" alisema Mbeto.

0 Comments