Na Mwandishi Wetu, Karatu
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea na programu ya kutoa elimu ya uhifadhi shirikishi na kuhamasiha utalii wa ndani kwenye shule mbalimbali ambapo leo tarehe 20 Novemba, 2025 watumishi wa Mamlaka hiyo wametembelea Shule ya Sekondari Banjika iliyopo Karatu Mkoani Arusha.
Katika ziara hiyo, wataalam wa uhifadhi na utalii walitoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi, vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro, pamoja na nafasi ya wanafunzi kuwa mabalozi wa utalii na uhifadhi ikiwemo kuanzisha klabu za uhifadhi wa mazingira.
hiyo kuanzia 2005 imetolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuomba Uongozi wa Mamlaka hiyo kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi na utalii kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ambao hupelekea elimu hiyo kwa wazazi wao wanaporudi nyumbani na hivyo kuhamasisha utalii wa ndani na utunzaji wa mazingira



0 Comments