Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi anasema katika Baraza la Mawaziri alilolitangaza 13 Oktoba 2025, Ikulu, Zanzibar alisema kuna nafasi nne za Uwaziri ambazo zinasubiri kujazwa ndani ya siku 90 na mawaziri wateule kutoka ACT Wazalendo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi alizitaja wizara hizo kuwa ni pamoja na wizara mama ya Uchumi wa Zanzibar ya Utalii na Mambo ya Kale, Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda na Wizara ya Afya.
Alisema uteuzi huo umezingatia mambo mengi ikiwa ni pamoja na uwiano wa pande zote mbili Unguja na Pemba.
Alibainisha kuwa ameitoa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa chama hicho cha ACT ili kumpa nafasi nzuri kiutendaji Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye pia atatokea chama hicho cha upinzani.
.jpg)
.jpg)
0 Comments