Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Chama cha Mapinduzi kimepongeza hotuba iliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ,Dk Hussein Ali Mwinyi yenye nia ya kuendeleaza maridhiano ya Kisiasa na Umoja wa Kitaifa Zanzibar.
Aidha, CCM kinaona fahari kushuhudia Uchaguzi Mkuu ukimalizika salama na sasa ni wakati wa kuleta maendeleo na kuwaunganisha wananchi.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis mara baada ya Rais Dk Mwinyi alipomaliza kulihutubia Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) .
Mbeto alisema hotuba ya Rais Dk Mwinyi imeweka wazi kusudio la kuondoa mivutano na misuguano isio na ulazima katika jamii, kwani masuala hayo aghalabu hukwamisha kasi ya maendeleo . .
Mbeto alisema kutokana na uzalendo wa Rais ,ameweka bayana msimamo wa Serikali yake, alipoahidi kuyasimamia maridhiano na kulindaa amani, utulivu na umoja.
Aliwataka wanasiasa wa vyama vyote wawe na fikra ya kutoendeleza malumbano, mivutano na mabishanao ambayo kiuhalisia hayana tija wala faida baaada ya uchaguzi kumalizika.
'Kurasa za siasa , uchaguzi na ushindani wa hoja na sera majukwani sasa zimeshafungwa. Lazima tuwe tayari kudumisha umoja na kuzitafutia majibu changamoto za maendeleo ya jamii"alisema Mbeto.
Pia Mwenezi huyo alisema ni zamu ya wananchi kuanza kuvifuatilia vikao vya Baraza la Wawakilishi kwa lengo la kuwaona wawakilishi wao wakiihoji, kuibana na kuzisimamia wizara za serikali .
Wakati huo huo, Mbeto alisifu juhudi za Serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa hatua ya kuanzisha meza ya Maridhiano na vyama vya Siasa ili kufukia suluhu ya upatanishi.
Alisema uamuzi wa kufungua pazia la Maridhiano hayo kati Serikali na upinzani mara baada ya uchaguzi , azma ni kuhuisha na kudumisha ustawi wa Aman ,umoja ,Haki na Utawala wa sheria.
Mbeto ameuiita msimamo huo wa Rais Dk Samia ni thabiti na wenye hisia na nia ya kuendeleza uungwana na ustaarabu wa kisiasa nchini .
Msimamo wa Serikali yake ametangazwa na Makamo wa Rais Dk Emmanuel Nchimbi , aliposhiriki kikao cha Wakuu wa Nchi kupitia Kamati ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (sadc)
Katibu Mwenezi huyo aliutaja msimamo huo, una lengo la kuyatia rutuba mazingira ili yawe tulivu na salama, na kuchochea shime ya kudumisha Umoja kupitia meza ya mazungumzo .
"CCM kinampongeza Rais Dkt. Samia kwa msimamo wake kabambe. Kimsingi amezingatia maoni, ushauri na kusiliza sauti za wachache dhidi ya walio wengi ili wote kuwaweka pamoja " alisema Mbeto

0 Comments