CCM YAONYA WANAOPANDA CHUKI ZA MUUNGANO




Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeonya watu mbalimbali wakiwemo baadhi ya viongozi wanaopanda chuki kuhusiana na nafasi ya Rais wa Muungano wa Tanzania na kuwataka watambue kuwa yupo kwa mujibu wa katiba.

Akizungumza katika mahojiano na SK On line Tv, mjini Zanzibar Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema wakati akizungumza na Mtandao wa NK kuwa kuna watu hivi sasa wanaleta uZanzibari na uTanganyika.

Alisema toka Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, nafasi hiyo imeshikwa na Zanzibar mara mbili wakati maRais kutoka Tanzania Bara ni wanne na ilitokea hivyo kwa mujibu wa katiba na hakuna ambaye alihoji.

Alisema Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitokea Bara, alikuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Benjamin Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete kisha John Pom,be Magufuli

“Zanzibar imetoa wawili tu kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Rais Dkt. Ali Hassan Mminyi na sasa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan” alisema na kuongeza kuwa waTanzania wasiwasikilize wapiga kelele wanaotaka kuingiza nchi katika matatizo makubwa.

Alisema pande zote mbili zina haki sawa katika muungano kwa kuwa ziliunganika Jamhuri ya Zanzibar na Tanganyika zote zikiwa zenye mamlaka kamili, ikiwa ni maazimio ya chama cha TANU na Afro Shiraz, chini ya kaulimbiu isemayo Binadamu Wote ni sawa.

“WaTzania tujenge nchi yetu, Rais akitoka upande wowote apewe ushirikiano, tusikubali kugawanywa kwa kigezo chochote” alisema Mbato na kuongeza kuwa Zanzibar na Tanganyika zimeunganishwa na undugu uliopo baina ya pande zote mbili.

Post a Comment

0 Comments