MBETO: ACT KINA SERA HATARI ZA UKABILA NA UBAGUZI

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimesema ACT Wazalendo kina ajenda ya siri na sera za ubaguzi hivyo ni hatari kwa mustakabali wa amani ya Zanzibar na watu wake ikiwa siku kitapata bahati kikachaguliwa kushika dola.

Mbeto alisema hayo kufuatia hatua ya Makamu Mwenyekiti wake Ismail Jussa Ladhu, kumshambulia jukwaani mgombea Urais wa CCM, Rais Dk Hussein Ali Mwinyi akidai hana asili ya Zanzibar ni ushahidi tosha ACT si chama sahihi kwa mustakbari mwema wa Zanzibar.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis , aliyesema ACT kina Sera za kibaguzi na ubaguzi ni hatari kwa ustawi wa umoja na mshikamano wa Kitaifa. 

Mbeto alisema karibu wananchi wote wa Zanzibar aidha watakuwa na asili moja ya Zanzibar na nchi nyingine.

Katika moja ya mikutano ya kampeni za uchaguzi hivi karibuni wa ACT, Jussa alidai kuwa chama chake kikishinda Urais, watu wasio na asili ya Zanzibar watarudishwa kwenye asili zao na kudai mmojawapo ni Rais Dkt. Hussein Mwinyi ambaye alidai kwao ni Mkuranga, mkoa wa Pwani, Tanzania Bara.

Mbeto alisema huo ni ubaguzi mpya ambao hautoi taswira njema kwa Zanzibar.

Akitoa mfano alisema kwa Zanzibar ni kisiwa cha watu wenye asili mchanganyiko na rangi mbalimbali (Cosmopolitans), hivyo atawaondoa watu wangapi na kuwaacha wangapi.

"Jussa amekuwa akimnyooshea kidole Rais Dk Mwinyi na kudai ana asili ya Mkuranga Tanzania Bara. Cha ajabu Jussa hataji asili yake ambayo ni India?" alihoji Mbeto.

Alisema kuwa mtu mwenye asili ya Mkuranga na India yupi aliyetoka nje ya Bara la Afrika.

Aidha alisema katika dunia ya sasa ambayo muafrika amezaa na mJapani, kuna waChina na Mgoa waliozaliwa Zanzibar na mtu mwenye asili ya Rwanda na Malawi amekuwa Rais wa Kwanza Zanzibar, madai ya Jussa ni zaidi ya upuuzi. 

"Zama ya ubaguzi wa rangi asili na ukabila imekwisha duniani. Kiongozi anayebagua wenzake kwa rangi, kabila au asili ni katili kuliko kiongozi wa zamani Afrika Kusini Pick Botter " alieleza.

Mbeto alidai Jussa ni mwanasiasa aliyeshindwa kujenga hoja za kisiasa na sasa anahubiri ubaguzi. 

'Hutamsikia hata siku moja akinadi sera za chama chake jukwaani anachokijua ni mtamko ya ubaguzi, wivu na chuki binafsi " alisema katibu mwenezi huyo.

Post a Comment

0 Comments