Viongozi wa Serikali, Wawekezaji wa Sekta ya Madini, na Wananchi wa Mahenge wanaendelea kuwasili katika eneo la Makanga, Mahenge Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro kwa ajili ya kushiriki Hafla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Mgodi wa Kinywe - Mahenge.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (MB), ambaye anatarajiwa kuzindua rasmi ujenzi wa mradi huo mkubwa unaotekelezwa na Kampuni ya Faru Graphite Corporation.
Hafla hiyo inaashiria kasi ya utekelezaji wa maono ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kukuza uchumi kupitia uwekezaji wa kimkakati kupitia Madini Muhimu.
Habari Kamili Itawajia Baadaye.
📍 Mahenge, Wilaya ya Ulanga
📅 Oktoba 9, 2025





0 Comments