Mageuzi hayo ambayo yameiingiza Zanzibar katika matumizi ya kidigitali katika sekta zote za mapato ya serikali pia yameongeza pato la Taifa kwa asilimia 278 ndani ya kipindi bhcho cha miaka minne na kuifanya uwepo udhibiti wa mfumuko wa bei na kuchangia ukuaji wa sekta za utalii, kilimo na uvuvi.
Rais Dkt. Mwinyi akizungumza leo 20 Oktoba 2025, wakati wa hafla ya kumpongeza, ugawaji wa gawio kwa wanahisa waliowekeza Zanzibar Skuk ambayo inafuata sharia za dini ya kiislam na uzinduzi wa Skimu ya Hifadhi ya Jamii ya Kiislamu (ZSSF), alisema mageuzi hayo yamekuwa msingi muhimu unaoijenga Zanzibar.
Dkt. Mwinyi alisema, fedha zilizowekezwa Zanzibar Skuk ndio ambayo yameiwezesha serikali kugharamia miradi ya kimkakati na kutoa gawio la kwanza leo ikiwa ni ndani ya miezi sita kama sheria ya huanzishwahji kwake inavyoeleza kuwa itatoa gawio kwa wawekezaji walionunua hisa hizo zisizo na riba kila baada ya miezi sita.
“Utoaji wa gawio la kwanza kwa wawekezaji ni ishara ya uwajibikaji na uadilifu katika kusimamia dhamana za Taifa” alisema na kuongeza kuwa Bima hizo na Skimu iliyozinduliwa ya hifadhi ya jamii za kiislamu hatua hiyo inalenga kujenga Zanzibar ya haki, ustawi na usawa wa kijamii.
Dkt. Mwinyi ambaye anagombea kwa awamu nyingine nafasi ya Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu 29 Oktoba mwaka huu 2025, alisema utoaji wa gawio kwa wawekezaji wa Skuk unaonyesha mageuzi mapya ya kiuchumi yaliyotekelezwa na serikali ambayo yamekuwa msingi muhimu wa kuijenga Zanzibar mpya inayowashirikisha wananchi katika kuijenga nchi.
Alisema Dkt. Mwinyi kuwa serikali yake itaendelea kutumia mifumo ya kidigitali na awali akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Fedha na Uchumi Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya alisema matumizi ya mikfumo ya kidigitali katika matumizi ya manunuzi ya serikali, kandarasi na utekelezaji wa miradi kumekuwa na mafanikio makubwa, uwazi na udhibiti wa fedha za serikali.
“Kabla ya 2021 kandarasi ya barabara hadi kutolewa na pengine malipo kufanywa kwa mkandarasi kungechukua hadi miaka mitatu lakini sasa ndani ya wiki mbili tu.” alisema Mkuya na kuongeza kuwa mfumo huo wa kikdigiti upo pia kwenye sekta za afya, uwezeshajhi na huduma zingine.



0 Comments