KUMBUKUMBU YA DKT. JANE GOODALL NA TANZANIA

Dkt. Jane Goodall enzi za uhai wake akiwa na kundi la vijana wanafunzi alioshirikiana nao kuanzisha Roots and Shoots jijini Dar es Salaam. Baadhi ya vijana hao walikuwa wanafunzi wanne wa Shule ya Sekondari Tambaza: Balozi Mobhare Matinyi (wa tatu kutoka kulia waliosimama), Dkt. Jan Masesa (wa nne kutoka kushoto waliosimama), Marehemu Jackson Mwandiki (wa pili kulia waliosimama) na Lazaro Swai (wa kwanza kulia waliosimama). Hii ilikuwa nyumbani kwake Msasani, jirani na kwa Mwalimu mnamo mwaka 1991 wakati akisherehekea miaka ya 30 ya utafiti mrefu zaidi duniani wa bila kukatisha wa wanyama. Mama huyu Mwingereza Jane alikuwa ametafiti wanyama aina ya sokwe mkoani Kigoma katika hifadhi ya Gombe. Leo dunia inaomboleza kifo chake kilichotokea tarehe 1 Oktoba, 2025, huko California, Marekani.

Post a Comment

0 Comments