DKT. MWINYI:KILA MMOJA ANAWAJIBU KUTUNZA AMANI


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mgombea nafasi ya Rais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametaka kila mwananchi kila mmoja kuitunza amani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu hapo 29 Oktoba 2025.

Akizungumza wakati wa Dua Maalum kuliombea Taifa iliyofanyika Masjid Mushawwar, Muembe Shauri leo 17 Oktoba 2025, Dkt. Mwinyi alisema dua kama hizo pamoja zizidi kufanyika na hata kila mmoja binafsi kuomba dua ili Mwenyezi !ungu aweze kuivusha nchi salama.

"Kila mmoja ana wajibu wa kuitunza amani yetu, kila mmoja amue hilo linamhusu" alisema. 

Alibainisha kuwa kila mtu achunge kauli na vitendo vyake ili asiwe sababu na chanzo cha uvunjifu wa amani nchin.

"Kauli za mtu au vitendo vyale vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani" alisema na kuongeza kuwa kila mmoja ajitahidi kuwa raiaa mwema.

Dkt. Mwinyi alisema ambalo hana shaka nalo ni kuwa akipewa awamu nyingine atafanya mambo mengi zaidi ya maendeleo na alitaka wagombea wenzake wakubaliane na matokeo kwa kuwa wengi wape.

"Tukubali matokeo yatakayotangazwa kwani wengi wape na sio lazima iwe wewe tu hata kama sivyo" alisema Dkt. Mwinyi ambaye aliambatana na viogozi mbalimbali wa kiTaifa akiwemo Rais Mstaafu, Dkt. Ali Mohamed Shein.

Awali Sheikh Farid Mfaume kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar alisema kuwa amani ndio msingi wa ustawi na vurugu daima huleta uharibifu jambo ambalo waTanzania wanapaswa kujiepusha nalo.

Post a Comment

0 Comments