Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa CCM imeendesha kampeni za kistaarabu na kuyafikia makundi yote ya kijamii nchini, hivyo ina kila sababu ya kushinda uchaguzi.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 24 Oktoba 2025, alipohutubia katika Mkutano Mkubwa wa Kampeni wa Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika Uwanja wa Mnazi Mmoja, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito kwa Wana-CCM na wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kukichagua Chama Cha Mapinduzi ili kipate ushindi mkubwa.
Aidha, amesema kuwa ushindi wa CCM unamaanisha kulindwa kwa Muungano wa Tanzania, Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na kudumisha umoja, amani na mshikamano wa Watanzania.


0 Comments