WAKILI KIPANGULA AMKABIDHI MKUU WA PDPC INNOCENT MUNGY PRESS CARD YA JAB

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amemkabidhi Kitambulisho cha Uandishi wa Habari Bw. Innocent Mungy, Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), baada ya kukidhi vigezo vinavyohitajika kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kitambulisho hicho leo, tarehe 03 Septemba 2025, katika ofisi za Bodi zilizopo Mtaa wa Jamhuri, Jijini Dar es Salaam, Bw. Mungy alisema ana furaha ya kuendelea na safari yake ya kitaaluma akiwa mwandishi wa habari aliyeambatana na ithibati ya Kisheria.

“Ninashukuru kwa heshima hii na nimejizatiti kutimiza wajibu wangu kwa weledi na uadilifu. Ithibati hii ni njia ya kuendelea kutoa taarifa sahihi, kwa dhamira ya kujenga uaminifu kwa umma,” alisema Bw. Mungy.


Aidha amewahimiza Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kupata ithibati ili kuongeza uwajibikaji na uadilifu wa taarifa zinazotolewa kwa umma.

“Kwa kuwa na ithibati, itakuza uwajibikaji na kuimarisha uaminifu wa taarifa zinazotolewa na taasisi za serikali.

#presscardkidijitali 

#najivujiapresscardyangu 

#ithibatitz

Post a Comment

0 Comments