Mgombea wa Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaomba
wananchi wa mkoa wa Mtwara wamchague ili serikali iendelee kuboresha na kupanua uwezo wa bandari ya Mtwara.
Ameeleza kuwa maboresho
yaliyofanyika tayari yameifanya bandari hiyo kuwa lango muhimu la biashara
kwa ukanda wa kusini, na kwamba hatua zaidi zitachukuliwa ili mazao ya
biashara kama korosho yasafirishwe moja kwa moja kutoka Mtwara kwenda
masoko ya kimataifa.
Dkt. Samia pia amesisitiza umuhimu wa bandari ya Mtwara kama kituo pekee
kinachosafirisha makaa ya mawe nchini, jambo linaloiongezea nafasi kubwa
katika uchumi wa taifa.
Ameahidi kuwa endapo ataendelea kuongoza,
serikali yake itawekeza katika miundombinu na huduma za bandari hiyo,
sambamba na kurahisisha upatikanaji na usafirishaji wa pembejeo za kilimo
kwa wakulima wa korosho.

0 Comments