TISEZA YAITA WAZAWA KUWEKEZA KWALA

Kaimu Meneja Uhusiano  na Mawasiliano  kwa  Umma  Mamlaka ya  ya Uwekezaji  na Maeneo  Maalumu  ya Kiuchumi  Tanzania (TISEZA) Adrina   Rushakya  amesema  kuwa wanawakaribisha wawekezaji  wazawa pamoja na wageni katika eneo hilo ambapo muhusika atapewa ekari moja bure.

Rushakya ametaja maeneo mengine ya uwekezaji ni Nala Dodoma ekari 607, Bagamoyo  Mkoani Pwani ekari 154   na Buzwagi Mkoani Shinyanga ekari 1,333 maeneo haya ya uwekezaji tauari yamenunuliwa. 

Akizungumza  katika ziara ya siku moja iliyofanyika katika eneo lenye ukubwa wa ekari 100 linalomilimiwa na  TISEZA Rushakya amesema kuwa  milango iko wazi  huku Ofisi  yao iko wazi  kwa ajili ya kuwahudumia wawekezaji ambao watafika ili kupata  taarifa  za utaratibu  wa kuwekeza katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na 

upatikanaji wa huduma za Brela, NIDA na huduma zingine muhimu zinazohusiana na uwekezaji sambamba na Mamlaka ya Mapato TRA (VAT),OSHA na  TBS

Akizungumza  leo tarehe 30 Septemba 2025 Rushakya amesema kuwa  muekezaji atapewa ekari moja bure ili aweze kujenga kiwanda  katika eneo hilo na kwa wale ambao wataonesha nia na kupewa eneo watapaswa kuliendeleza ndani ya mwaka mmoja.

"Mpaka sasa tayari wawekezaji  wazawa kumi wamejitokeza ambapo wamebainisha kuwa watajenga viwanda vya kilimo, sola  na bidhaa za majumbani" amesema 

Rushakya.

Aidha  ameongeza  kwa kusema kuwa sharti la muekezaji atatakiwa  kuwa na mtaji wa dola za Kimarekani  Bilioni tano huku muekezaji wa kigeni atatakiwa  kuwa na mtaji wa Bilioni kumi.

Wakati huohuo Rushakya aliongoza Waandishi wa Habari kutembelea kiwanda cha majokofu ambapo ilielezwa kuwa kwa siku kina uwezo wa kutengeneza majokofu 100 hadi 150 huku yale makubwa yenye milango miwili hutengezwa kumi kwa siku .

Post a Comment

0 Comments