Mjiolojia kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara, Godfrey Keraka, amesema kuwa kila jiwe lina thamani kwa sababu ya mchango wake katika sekta ya madini, maendeleo ya taifa na teknolojia ya kisasa duniani.
Akizungumza kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Keraka ameeleza kuwa sekta ya madini inachangia asilimia 10.1 ya Pato la Taifa (GDP) na ni urithi muhimu wa nchi unaopaswa kulindwa.
Kwa upande mwingine, makaa ya mawe yametajwa kuwa chanzo muhimu cha nishati, huku dhahabu na fedha zikibainishwa kama madini yenye thamani kubwa yanayotumika katika hifadhi ya fedha, mapambo, sarafu na vifaa vya kielektroniki.
Keraka pia amesisitiza umuhimu wa graphite na lithium kama madini ya kimkakati katika utengenezaji wa betri na mifumo ya kuhifadhi nishati.
“Wananchi wanapaswa kuelewa kuwa kila jiwe lina thamani kubwa. Miamba na madini ni urithi wa taifa unaopaswa kulindwa na kutumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho,” amesema Keraka.
Keraka pia amesisitiza umuhimu wa graphite na lithium kama madini ya kimkakati katika utengenezaji wa betri na mifumo ya kuhifadhi nishati.“Wananchi wanapaswa kuelewa kuwa kila jiwe lina thamani kubwa. Miamba na madini ni urithi wa taifa unaopaswa kulindwa na kutumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho,” amesema Keraka.




0 Comments