KASACO MEDIA YAZINDULIWA WA KISHINDO DAR


REDIO ya Mtandaoni inayofahamika kwa jina la KASACO CO TZ yenye maskani yake Tabata Mawenzi Jijini Dar es Salaam imezinduliwa leo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Meneja wa Redio hiyo Emmy Mwaipopo amesema kuwa redio hiyo ambayo hapa ni tawi huku makao makuu yako Mkoani Kigoma imeanzishwa kwa kuzingatia misingi ya uwazi , uadilifu, na kujitolea katika misingi ya kukuza maendeleo katika jamii na uchumi kwa kutumia maarifa ya kisasa , ushirikiano wa kimataifa na teknolojia. 
Meneja Emmy amesema kuwa Redio hiyo ina matarajio ya kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi , KSACO CO TZ Limited inalenga kuwa chombo imara cha maendeleo endelevu kupitia miradi ya kijamii, ujasiriamali, mafunzo , uzalishaji wa maudhui na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii.

"Kampuni inasimamiwa kwa weledi na timu ya viongozi wabobevu ambao wanaingozwa na maadili ya kazi yenye maono ya mbali" amesema Mwaipopo. 

Amesema kuwa KASACO inajivuia kuwa na muundo shirikishi wa umiliki unaojumuisha raia wa Tanzania na washirika kutoka nje ya nchi ,hali inayosaidia kuimarisha mtazamo wa kimataifa bila kupoteza mwelekeo wa ndani.
"Kwa misingi huu Kampuni imejizatiti kutoa huduma zenye viwango vya juu kwa mujibu wa sheria , taratibu na kanuni zinazotambulika ndani na nje ya nchi" amesisitiza Mwaipopo.

"KASACO dira yake ni kuwa Kampuni inayoongoza katika Ukanda wa nchi zilizoko Afrika Mashariki na kutoa huduma za kijamii, maendeleo ya ujasiriamali na uzalishaji wa ubunifu unaoleta mabadiliko chanya katika jamii" amesema Mwaipopo.

Aidha vipindi vitakavyokua vinakwenda hewani ni pamoja na taarifa ya Habari, Makala , Mahojiano na Mijadala tofauti tofauti. 
Pia kutakua na vipindi vya burudani ambavyo ni muziki, utamaduni,
michezo uchambuzi na vingine mbalimbali.
Kauli mbiu ya KASACO Media inase Tunaangazia Maisha ,Tunaandika kesho.

Post a Comment

0 Comments