DKT.MIGIRO AZINDUA PROGRAMU YA MAFUNZO KWA VIONGOZI


Katibu Mkuu wa Chama Cha  Mapinduzi (CCM) Dkt. Asha Rose Migiro amesema Tanzania
 imejipanga vyema kwa zoezi la uchaguzi mkuu ujao, na kusisitiza kuwa kila kitu kipo katika kuhakikisha taifa linadumisha amani wakati na baada ya uchaguzi.

Amesema hayo wakati akizindua programu za Shahada za Uzamili na Uzamivu kuhusu Utawala kwa mwaka wa masomo 2025/2026 zitakazoendeshwa kwa pamoja na Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha (MJNLS) iliyoko  Manispaa ya Kibaha na Shule ya Uongozi ya Renmin Global ya China.

Migiro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shule hiyo ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere.

Akizungumza  na Waandishi  wa habari mara baada ya ufunguzi wa Programu hiyo  Dkt. Migiro amesema hatua hiyo ni muendelezo wa urafiki wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili na vyama viwili vya CCM na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) cha China ambavyo vimethaminiwa na pande zote mbili.

"Pande hizi mbili zina historia ndefu ya urafiki ambayo imeleta mabadiliko chanya kwa pande zote mbili. Tukio la leo ni alama ya hatua nyingine muhimu ya uhusiano huu", amesema Dkt.Migiro. 

 Wakati akimkaribisha Katibu Mkuu, Waziri Mkuu wa zamani  Mizengo Pinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya MJNLS, ametoa wito kwa makundi ya vijana kuelekezwa zaidi kwa mafunzo ili kuwawezesha kuwa viongozi wazuri wa baadaye.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Tamzania, Chen Mingjian amesema kuwa China iko tayari na imejitolea sana kudumisha uhusiano wa urafiki  wake na Tanzania na kubadilishana uzoefu na wataalamu wake katika nyanja mbalimbali za maendeleo. 

 "China ina nia ya dhati ya kubadilishana uzoefu na maendeleo yake katika teknolojia kwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika ili kuziwezesha kupata maendeleo katika teknolojia ya kisasa na hasa katika matumizi ya Akili za Bandia (AI) katika nyanja za biashara, viwanda, biashara na nyinginezo ili kuongeza uzalishaji," amesema.

 Prof. Wang Wen- Mkuu wa Taasisi ya Masomo ya Kifedha ya Chongyang katika Chuo Kikuu cha Renmin, amesema kuwa Chuo Kikuu hicho ni mojawapo ya vyuo vikuu bora zaidi nchini China ambacho kimeanzishwa mwaka wa 1937.

Kozi zitakazotolewa zimeundwa kukidhi mahitaji.

 Wakati wa hafla hiyo, Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Renmin Prof. Zhang Donggang na Lin Shamgli- Rais wa Chuo hicho walituma salamu

zao kupitia simu ya video na kuahidi kuendeleza uhusiano na Shule.

Mkuu wa Shule JMNLS Prof. Marcellina Chijoriga amesema  kuwa shule hiyo imekuwa na uhusiano mzuri na Chuo Kikuu cha Renmin na kuongeza kuwa kuanza programu za Uzamili na Uzamivu kutaimarisha urafiki baina yao.

 "Jumla ya wanafunzi 32 kutoka nchi sita ambazo zinamiliki Shule hii- Tanzania, Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia na Afrika Kusini wataanza kusoma kozi hizi. Wanafunzi 10 watasomea digrii za Uzamivu na wengine 22 watasomea Shahada za Uzamili", amefafanua Chijoriga. 

 Aidha Prof. Chijoriga ameongeza kuwa huu ni mwanzo wa sura mpya katika shule hiyo ambayo ilikuwa ikitoa kozi fupi tangu ilipoanzishwa mwaka wa 2022.

Post a Comment

0 Comments