KOKA: TUTAKATISHE MIOYO CCM IKASHINDE KWA KISHINDO


Mbunge mteule wa Jimbo la Kibaha  Mjini Mhe.Silvestry Koka ametoa rai kwa wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM  kujitokeza  kwa wingi siku ya uchaguzi  na kuchagua Mbunge  na Madiwani  wa CCM. 

Pia amesema kuanzia sasa ndiyo muda muafaka wa kusafishana nyoyo na kwenda kusaka ushidi wa kishindo kwa CCM. 

"Sisi tunarekodi nzuri ya msingi mzuri  na imara na tuliujenga kwenye kuajiandikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa na tulishinda kwa kishindo,hatuna uoga wa kushinda na namba yetu ikabaki palepale namba moja.

Koka amesema hayo leo tarehe 25 Agosti 2025 alipozungumza kwenye mkutano na wanachama na wananchi  wa Jimbo la   Kibaha Mjini  kwenye mkutano uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Wilaya CCM Kibaha Mkoani Pwani mara baada ya kuchukua  fomu.

Mhe.Koka amesema kuwa Madiwani wengine watachaguliwa kutoka Mbawa ,Visiga ,Misugusugu, Kongowe   ,Viziwaziwa  ,Mkuza ,Kibaha ,Msangani ,Pangani, Tangini ,Mailimoja  ,Picha ya Ndege, Tumbi na Sofu.

Koka anatarajiwa kurudisha fomu hiyo tarehe 27 Agosti 2025 ambapo atakua tayari kwa  kuanza kampeni za uchaguzi mkuu ujao  utakaofanyika tarehe 29,Oktoba 2025

Aidha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Kibaha Mwalimu  Mwajuma Nyamka amesema kuwa anawasisitiza  wananchi kwamba  mgombea kiti cha ubunge Koka na Madiwani  wote wa Kata 14 wanapata kura za kutosha  katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika tarehe 29 Oktoba  2025.

"Twendeni  tukazitafute kura za Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kwa umoja wetu  ni imani yangu kwamba kwa mkusanyiko mliojitokeza kwa muda mfupi  tunasubiri kuthibitishwa.

"Kipekee nimefurahishwa kuwaona wagombea ambao walitia nia katika kuwania nafasi ya Ubunge na mgombea wetu wako hapa tangu asubuhi  tumetembea nao nawapongeza na nawashukuru  sana wameturahisishia kazi ta kwenda kutafuta kura za CCM,wamemwaga mambo hadharani kwamba chama kwanza  mtu baadaye"amesema Mwalimu Nyamka.

Chama kimetuletea wagombea wewe nani bado unabaki na vinyongo twendeni tukavunje makundi na makundi yanavyunjwa na  walioshinda  kaacheni majigambo ambayo yatawapa wengine  unyonge, wakati wa mchakato  mambo mengi yamepita  lakini  lengo lao wote walikua wanatafuta nafasi kuwania kiti cha Ubunge yaliyopita si ndwele tugange yajayo" amesisitiza  Nyamka.

"Kuanzi leo mkikuta kuna  mtu anaendeleza kumchafua mtu huku na yeye ni mwanachama basi mjue huyo hayuko sawa" amesema Nyamka.

Wakati huohuo wakizungumza katika nyakati tofauti   kwenye hadhara hiyo  aliyekua mtia nia Mussa Mansuri amesema  katika uchaguzi huo watia nia na mgombea wamefanya mazoezi, tunawapongeza wagombea wote  waliopita.

"Koka ni Jemedari  wa Jimbo la Kibaha Mjini  hivyo nawaomba ndugu zangu  nguvu zote  tuhakikishe  tunaelekeza  katika kukipigania Chama Cha Mapinduzi

(CCM) ,"naahidi  ndani  ya moyo wangu  wewe ndiyo dira  yetu na wewe ndiyo wa kutuunganisha  na unatakiwa  uwe Kiongozi mlezi" amesema Mansuri.

Aidha naye aliyekua mtia nia Mwalimu  Abubakar  Alawi amesema kuwa "Tumeua makundi yote wachawi wote  tupa kule hakuna cha ajabu tutakwenda kushinda  kwakishindo twende tukawaambie  watu tumesimamana Koka na niko tayari kuunga juhudi zote za Chama Cha Mapinduzi (CCM)" amesema Alawi. 

Post a Comment

0 Comments